FAHAMU JINSI YA KUOMBA SALA YA VITA
SALA YA VITA (0766500747)
Namuungamia
Mungu Mwenyezi kutokana na dhambi zangu zote nilizokutenda Bwana kwa mawazo
yangu, kwa vitendo vyangu na kutotimiza wajibu wangu, Bwana unisamehe, naomba
msamaha wa dhambi zangu kwa jina takatifu la Yesu Kristo Mwokozi wangu,
natangaza uhuru wangu kwa damu ya Yesu Kristo wa Nazareth.
Nakuja
kwa Baba Mtakatifu, Mungu wangu katika jina takatifu litetemeshalo mpaka kuzimu
la Bwana wetu Yesu Kristu, naomba unijalie moyo wa ujasiri, nguvu na imani
katika sala hii, nipe ujasiri kama mtumishi wako Daudi katika vita na Goliati,
univalishe nguvu na imani kutoka mbinguni kwa msingi wa neno lako.
Sasa
Mwenyezi Mungu natumia moyo wa ujasiri, nguvu na Imani uliyonijalia kupiga na
kuteketeza milele mipango yote ya shetani na mawakala wake dhidi yangu, na
dhidi yah ii kazi yangu na familia yangu yote katika jina la Yesu Kristo.
Baba
nipe mpako wa kivita kama uliompa Daudi zaburi 89:20-24 inashuhudia na ahadi
yako yasema “mimi nitawaponda wapinzani wake, nitawaangamiza wote wanaonichukia”
kwa neno hili Mwenyezi Mungu nawakabidhi maadui zangu wote mbele yako.
Baba
Mungu Mwenyezi navaa silaha za vita kama ilivyoandikwa (waefeso 6:10-18) navaa
ukweli kama mkanda kiunoni mwangu, navaa uadilifu uwe kama vazi la kujikinga
kifuani, hamu ya kutangaza habari njema na amani iwe kama viatu miguuni pangu,
imani iwe ngao mikononi mwangu kama kofia ya chuma na neno la Mungu kama upanga
niliopewa na roho Mtakatifu dhidi ya maadui zangu.
Nathibitisha
neno la Mungu ni kweli na nachagua leo kuishi katika mwanga wa neno hilo,
fungua macho yangu Bwana unionyeshe maeneo ya maisha yangu yasiyokupendeza na
maadui wangu wote waangaziwe nuru yako, na ninabomoa leo katika maisha yangu
makao yote ya shetani na kuangamiza mipango yote ya shetani ambayo ameipanga ndani
yangu, ameijenga ndani yangu dhidi ya akili yangu, afya yangu, taaluma yangu,
kazi yangu, mme wangu, utashi wangu, maeneo yangu, hisia zangu na mwili wangu.
Navaa
mamlaka Bwana kwa neno lako toka Mathayo 18:18 ninatuma neno hili kufunga nguvu
zote za shetani na mawakala zake wanaojidhihirisha katika maisha yangu kwa jina
la Yesu Kristo, nawafunga na kuwagombanisha wao kwa wao mpaka watakapokiri kwa
vinywa vyao na matendo yao kuwa Yesu Kristo ni Bwana.
Nateketeza
nguvu zote za giza katika kazi yangu na nyumbani ninamoishi na eneo lote bila
kujali zimejificha wapi iwe hewani, angani, motoni, ardhini, baharini, chini ya
bahari, chini ya ardhi naziteketeza zote kwa jina la Yesu, nakuja kinyume na
pepo wakuu wote wa uovu katika nchi hii, mji huu, nyumba hii na katika eneo
langu la kazi kwa jina la Yesu Kristo.
Nafunga
mapepo yote na nguvu yote ya kishirikina na uchawi inayotumika na watu hawa
walioumbwa kwa sura ya mfano wa Mungu, nafunga nguvu zako zote wewe (Taja
maadui kwa majina yao) na kundi lenu lote, nawaweka wote chini ya msalaba wa
Kristo katika jina la Yesu mpaka pale mtakapokili Yesu Kristo ni Bwana.
Kwa
nguvu za Mwenyezi Mungu nawatangazia msamaha kwa yale yote mlionitendea, maana
nguvu zako Mungu wangu na ulinzi wako umejidhirisha juu ya maisha yangu na kwa
jina la Yesu nakuja kinyume na kusanyiko lolote la kichawi katika eneo langu la
kazi, shule yangu, nyumba yangu kuanzia angani, motoni, ardhini, chini ya
ardhi, baharini, chini ya bahari, karibu na nyumba hii popote pale kwa jina la
Yesu Kristo.
Katika
jina tukufu la Yesu Kristo, nafunika mahali hapa na eneo hili kwa damu azizi ya
Bwana wetu Yesu Kristo, nafunika shule yangu kwa damu ya Yesu Kristo na damu ya
Yesu ikawateketeze roho za giza zote katika eneo hili, nafungulia moto war oho
mtakatifu ufunike eneo langu lote la kazi, nafungulia ulinzi wa Mungu katika
pembe zote za mahali hapa, naangamiza roho zote za visasi kwa jina la Yesu
Kristo.
Baba
mtakatifu nakupa sifa zote, heshima na utukufu, wafungulia malaika wako wenye
nguvu za kivita kushuka na kuweka ulinzi mahali hapa dhidi ya shetani na
majeshi yake ya nguvu za giza. Namwaga damu ya Yesu katika maeneo yote ya
nyumba hii na wapanga malaika wa Mungu kuyalinda maeneo yote ninamoishi kwa
jina la Yesu Kristo.
Baba
yetu x 3 salamu Maria x 3 atukuzwe x 3
Mtakatifu
Mikael Malaika Mkuu – utuombee
Mtakatifu
Raphael Malaika Mkuu – Utuombee
Watakatifu
Malaika Wakuu – utuombee
Amina.
UNAWEZA PIA KUTAZAMA VIDEO HIZI ZA SAUTI KWAJILI YA MAFUNDISHO ZAIDI
Maoni
Chapisha Maoni