ROZARI YA KUWAOMBEA MAREHEMU TOHARANI

 


ROZARI YA KUWAOMBEA MAREHEMU TOHARANI.

 

*• Jinsi na namna ya kusali.*

*(Tumia Rozari ya kawaida)*

 

Anza Rozari kwa kupiga Ishara ya Msalaba huku ukisema: "Kwa Jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina".

 

Kisha sema maneno haya:

K. Ee Mungu utuelekezee msaada.

W. Ee Bwana utusaidie hima.

Atukuzwe Baba....

 

SALA YA MWANZO

"Ee Majeraha ya Bwana wetu na Mtukufu sana, ambayo yalimgharimu uchungu na damu. Ee Majeraha yenye utukufu, ambayo yalikuwa asili ya mapendo yake yasiyo na mwisho kwa ajili yetu. Tunakusihi utuonee huruma sisi na roho zote wanaoteseka Toharani na hata wakosefu wote maskini walioko duniani. AMINA"

 

*• Kwenye punje kubwa: Sali SALA YA ATUKUZWE BABA...*

 

(Baada ya hapo, sala ya Mtakatifu Getruda Mkuu isaliwe)

 

SALA YA MTAKATIFU GETRUDA MKUU.

"Baba wa milele, ninakutotelea damu yenye thamani kuu ya Yesu Mwanao Mungu, nikiunganisha na sadaka za Misa Takatifu zinazoadhimishwa leo popote duniani. Kwa ajili ya roho za marehemu Toharani, kwa ajili ya wakosefu wote duniani, kwa ajili ya Wakatoliki walio wakosefu, kwa ajili ya wakosefu wa nyumbani kwangu mwenyewe na wale wa familia yangu. AMINA".

 

• Kwenye punje ndogo kumi (10):

K. Raha ya milele uwape ee Bwana.

W. Na mwanga wa milele uwaangazie, marehemu wote wapumzike kwa amani. AMINA.

 

SALA YA MWISHO

K. Ee Bwana usikie sala yangu.

W. Na mlio wangu ukufikie.

K. Marehemu wote wapumzike kwa amani.

W. AMINA

 

TUOMBE

"Baba wa milele Muumba na Mkombozi wa waamini wote, tunaomba msamaha wa dhambi zote roho za watumishi wako huko Toharani. Ni hao ambao sala zetu tunazileta mbele yako, ili waweze kuopolewa kutokana na huruma yako ya milele. Na wapokee msamaha wako, ambao daima waliutamainia kwako. AMINA".

 

K. Roho Takatifu mliotoka Toharani.

W. Tuombeeni sasa na milele. AMINA.

 

LITANIA YA KUWAOMBEA MAREHEMU TOHARANI.

 

K. Bwana uwahurumie  marehemu, W. Bwana uwahurumie.

K. Kristo uwahurumie marehemu, W. Kristo uwahurumie.

K. Bwana uwahurumie marehemu, W. Bwana uwahurumie.

K. Kristo kwa wema utusikie, W. Kristo utusikilize.

 

Kiitikio (Uwahurumie marehemu)

Baba wa Mbinguni Mungu,

Mwana Mkombozi wa dunia Mungu,

Roho Mtakatifu Mungu,

Utatu Mtakatifu Mungu mmoja,

 

Kiitikio (Uwaombee marehemu)

Maria Mtakatifu,

Mzazi Mtakatifu wa Mungu,

Bikira Mkuu wa Mabikira,

Mama wa Mungu,

Mama wa Huruma,

Mlango wa Mbingu,

Wewe uliye Mfariji wa wanyonge,

Mtakatifu Yosefu,

Mtakatifu Mikaeli,

 

Kiitikio (Muwaombee Marehemu)

Enyi Malaika Watakatifu na Malaika wakuu,

Enyi Mababu wote na Manabii,

Mitume wote Watakatifu na Wainjili,

Wafuasi Watakatifu wote wa Bwana,

Watoto Watakatifu msio na hatia,

Mashahidi wote Watakatifu,

Maaskofu na Waamini wote,

Waalimu Watakatifu wa Kanisa,

Mapadre wote na Mashemasi Watakatifu,

Enyi Wamonaki na Waheremita,

Mabikira na Wajane wote Watakatifu,

Enyi Watakatifu wote wa Mungu,

 

K. Uwarehemu W. Uwaokoe ee Bwana.

K. Uwarehemu W. Uwaopoe ee Bwana.

 

Kiitikio (Uwaokoe ee Bwana)

Katika maumivu yao yote,

Kutokana na hukumu yao kali,

Kutokana na wadudu wasiokufa wanaotafuna nafsi zao,

Kutokana na uchungu wao mkali,

Kutokana na kifungo chao cha mateso,

Kutokana na moto mkali unaowachoma,

Kutokana na mateso yao yasiyoelezeka,

Kutokana na adhabu zao zote,

 

Kiitikio (Uwaopoe ee Bwana)

Kwa kuchukua ubinadamu wako wa ajabu,

Kwa kuzaliwa kwako Kitakatifu,

Kwa Ubatizo na Mfungo wako Mtakatifu,

Kwa unyenyekevu wako mkuu,

Kwa utii wako mkamilifu,

Kwa umaskini wako wa kweli,

Kwa kuhukumiwa kwako bila hatia,

Kwa kubeba Msalaba wako kwa ukatili,

Kwa kusulubiwa kwako kwa ukatili mkuu,

Kwa kutelekezwa kwako katika mateso,

Kwa sadaka ya kifo chako Msalabani,

Kwa Majeraha yako matano Matakatifu,

Kwa kuchomwa Moyo wako Mtakatifu,

Kwa ufufuko wako Mtakatifu,

Kwa kupaa kwako kiajabu,

Kwa ujio wa Roho Mtakatifu Mfariji,

Kwa mastahili na maombezi ya Mama yako Mtakatifu,

Kwa mastahili na maombezi ya Watakatifu wote,

 

Kiitikio (Ee Bwana twakuomba utusikie)

Sisi wakosefu maskini,

Uweze kuwakinga na mateso roho walio Toharani,

Uweze kuwaopoa katika mateso yao machungu,

Uweze kuwashirikisha mastahili ya kazi zako zote kwa ajili yao,

Kwa msaada wa Mtakatifu Mikaeli Malaika Mkuu na Malaika wote Watakatifu watuongoze katika mwanga na heri ya milele,

Kwamba uweze kuwafurahisha mapema kwa kuja kuuona Uso wako wa milele,

Uweze kuwashirikisha mastahili ya kazi zote njema za Waamini wako,

Uweze daima kusikiliza sala zetu zote kwa ajili yao,

Uwajalie marehemu wazazi, watoto, ndugu, marafiki na wafadhili wetu heri yako ya milele,

Uwaopoe roho wale ambao kwa upande mwingine sisi tumeshiriki katika kosa la adhabu yao,

Kwamba uwe na huruma ya pekee kwa roho wote wasio na waombezi hapa duniani,

Uwajalie amani ya milele Wakristo wote marehemu,

Kwa maombezi ya Wakristo wote roho maskini uwajalie huruma na mapendo yako ya milele,

Yesu Mwana wa Mungu na Mfalme wa heri ya milele,

 

K. Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za ulimwengu, W. Uwakinge ee Bwana.

K. Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za ulimwengu, W. Uwaopoe ee Bwana.

K. Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za ulimwengu, W. Uwahurumie ee Bwana.

 

K. Pumziko la milele uwape ee Bwana,

W. Na mwanga wa milele uwaangazie, marehemu wote wapumzike kwa amani. AMINA.

 

*TUOMBE*

"Ee Mungu Bwana wa Maisha na kifo, uwaonyeshe huruma yako ya milele Watumishi wako waliokuwa Waamini wako na bado walikutamainia wewe siku zote. Uwajalie wote msamaha wa kosa la adhabu yao wanayoitumikia, uopoe roho zao kutokana na mateso yao makali huko Toharani. Kwa niaba yao, tunaomba kupitia Maombezi ya Bikira Maria na kwa njia ya Kristo Bwana wetu. AMINA".

 

Mwisho maliza Rozari kwa kupiga Ishara ya Msalaba kama ulivyofanya hapo mwanzo.

 

RAHA YA MILELE UWAPE EE BWANA...

 

 

 

 

 

………………………………………………………


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI YA KUSALI ROSARI TAKATIFU YA BIKRA MARIA

MALAIKA MKUU MT. MICHAEL UTULINDE KATIKA VITA

FAHAMU JINSI YA KUOMBA SALA YA VITA

SALA KWA AJILI YA KUFUNGULIWA KUTOKA KATIKA NGUVU ZA GIZA

HISTORIA YA MAISHA YA BIKIRA MARIA