JINSI YA KUSALI ROSARI TAKATIFU YA BIKRA MARIA
JINSI YA KUSALI ROSARI TAKATIFU YA
BIKRA MARIA
KANUNI ZA IMANI
1. Nasadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi muumba mbingu na dunia
na kwa Yesu Kristo mwanaye wa pekee, Bwana wetu, aliyetungwa kwa uwezo wa roho
mtakatifu akazaliwa na Bikra Maria akateswa kwa mamlaka ya Polystyo Pilato,
akasulubiwa akafa, akazikwa akashukia kuzimu siku ya tatu akafufuka katika wafu
akapaa mbinguni, amekaa kuume kwa Mungu baba Mwenyezi toka huko atakuja kwa
utukufu kuwahukumu wazima na wafu, Nasadiki kwa roho Mtakatifu, Kanisa takatifu
Katoliki, ushirika wa watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili na
uzima wa milele ijayo Amina.
2.
BABA YETU
Baba Yetu uliyembinguni jina lako litukuzwe, ufalme wako
ufike utakalo lifanyike duniani kama mbingui utupe leo mkate wetu wa kila siku,
utusamehe makosa yetu, kama tunavyo wasamehe na sisi waliotukosea usitutiye
katika kishawishi lakini utuokoe maovuni Amina.
3.
SALAMU MARIA
Salamu Maria umejaa neema Bwana yu nawe umebarikiwa
kuliko wanawake wote na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa, Maria mtakatifu
mama wa Mungu utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu Amina.
4.
ATUKUZWE
Atukuzwe Baba, Mwana na Roho Mtakatifu – Amina.
Pamoja na Rosari kuwa na
matendo 4, ambayo kila tendo yemebeba mafumbo 5, hivyo kabla ya kusali au
kutamka fumbo (tendo) sala zifuatazo zinatangulia kabla ya fumbo. Ukiwa
umeshika punje yako ya fumbo utasali,
-
Atukuzwe Baba x 1
-
Tuwasifu milele
Yesu, Maria na Yoseph x 1
-
Ee Yesu mwema
utusamehe dhambi zetu utukinge na moto wa milele ongoza roho zote mbinguni hasa
za wale wanaohitaji Zaidi huruma yako.
-
Damu ya Kristo
iziokoe roho zote toharani izijaliye nuru ya uzima wa milele – Amina
-
Tendo | fumbo (Hapa
unataja tendo \ fumbo )
-
Baada ya Tendo
utasali Baba yetu kabla ya kuanza tembe kumi za salamu Maria.
MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi)
Tendo la kwanza:
Malaika Gabriel anapasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu * Tumwombe
Mungu atujalie unyenyekevu.
Tendo la pili:
Bikra Maria anakwenda kumtembelea Elizabeth Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya
jirani.
Tendo la Tatu: Yesu
anazaliwa Bethlehemu* Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara.
Tendo la Nne: Yesu
anatolewa hekaluni* Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo.
Tendo la Tano: Maria
anamkuta Yesu hekaluni*
Tumwombe Mungu
atujalie kuwatii wakubwa wetu.
MATENDO YA UCHUNGU (Jumanne na Ijumaa)
Tendo la kwanza:
Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu.
Tumwombe Mungu
atujalie sikitiko la dhambi.
Tendo la Pili:
Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu.
Tumwombe Mungu
atujalie kuacha dhambi za uchafu.
Tendo la Tatu:
Yesu anatiwa miiba kichwa kwa ajili yetu.
Tumwombe Mungu
atujalie kushinda kiburi.
Tendo la Nne:
Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu.
Tumwombe Mungu atujalie
kuvumilia taabu.
Tendo la Tano:
Yesu anakufa Msalabani.
Tumwombe Mungu
atujalie kuwapenda Yesu na Maria.
MATENDO YA UTUKUFU (Jumatano na Jumapili)
Tendo la kwanza:
Yesu anafufuka.
Tumwombe Mungu
atujalie kugeuka watakatifu.
Tendo la Pili:
Yesu anapaa mbinguni.
Tumwombe Mungu
atujalie kwenda mbinguni.
Tendo la Tatu:
Roho Mtakatifu anawashukia Mitume.
Tumwombe Mungu
atujalie bidii katika dini yetu.
Tendo la Nne:
Bikira Maria anapalizwa mbinguni.
Tumwombe Mungu
atujalie kufa vizuri.
Tendo la Tano: Bikira
Maria anawekwa Malkia mbinguni.
Tumwombe Mungu
atujalie kudumu katika njia njema.
MATENDO YA MWANGA (Alhamisi)
Tendo la kwanza:
Yesu anabatizwa mto Yordani.
Tumwombe Mungu
atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.
Tendo la Pili:
Yesu anageuza maji kuwa divai huko kana.
Tumwombe Mungu
atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya Injili.
Tendo la tatu:
Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu.
Tumwombe Mungu
atujalie kupokea ufalme wake wa toba ya kweli.
Tendo la Nne:
Yesu anageuka sura.
Tumwombe Mungu atujalie
neema ya kuung`arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.
Tendo la Tano:
Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristi.
Tumwombe Mungu
atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine.
Kila baada ya
kumaliza kusali rosary Sali sala hii: SALAMU MALKIA
Salamu, Malkia, Mama
mwenye huruma, uzima, tulizo na matumaini yetu, salamu. Tunakusihi ugenini hapa
sisi wana wa Eva. Tunakulilia tukilalamika na kuhuzunika bondeni huku kwenye
machozi. Haya basi, mwombezi wetu, utuangalie kwa macho yako yenye huruma. Na
mwisho wa ugeni huu, utuonyeshe Yesu, mzao mbarikiwa wa tumbo lako. Ee mpole,
ee mwema, ee mpendevu, Bikira Maria.
·
Kumbuka fumbo
linatamkwa na mtu mmoja, mwongozaji na baada ya fumbo maombi au ombi katika
fumbo linaitikiwa na watu wote, kama unasali peke yako utataja na ombi wewe
mwenyewe kwa kila fumbo.
LITANIA YA BIKIRA MARIA
Bwana,
utuhurumie Bwana, utuhurumie
Kristo,
utuhurumie Kristo, utuhurumie
Bwana,
utuhurumie Bwana, utuhurumie
Kristo,
utuhurumie Kristo, utuhurumie
Baba wa Mbinguni,
Mungu utuhurumie
Mwana, mkombozi wa
dunia, mungu utuhurumie
Roho mtakatifu,
mungu utuhurumie
Utatu mtakatifu,
mungu mmoja utuhurumie
Maria mtakatifu utuombee
Mzazi Mtakatifu wa
Mungu utuombee
Bikira Mtakatifu
mkuu wa mabikira utuombee
Mama wa Kristo utuombee
Mama wa neema ya
Mungu utuombee
Mama mtakatifu
sana utuombee
Mama mwenye moyo
safi utuombee
Mama mwenye
ubikira utuombee
Mama usiye na
dhambi utuombee
Mama mpendelevu utuombee
Mama
msitaajabivu
utuombee
Mama wa shauri
jema utuombee
Mama wa Muumba utuombee
Mama wa kombozi utuombee
Bikira mwenye
utaratibu utuombee
Bikira mwenye
heshima utuombee
Bikira mwenye
sifa utuombee
Bikira mwenye
uwezo utuombee
Bikira mwenye
huruma utuombee
Bikira
mwaminifu utuombee
Kioo cha haki utuombee
Kikao cha
hekima utuombee
Sababu ya furaha
yetu utuombee
Chombo cha
neema utuombee
Chombo cha
heshima utuombee
Chombo bora cha
ibada utuombee
Waridi lenye
fumbo utuombee
Mnara wa Daudi utuombee
Mnara wa pembe utuombee
Nyumba ya
dhahabu utuombee
Sanduku la
agano utuombee
Mlango wa
mbinguni utuombee
Nyota ya
asubuhi utuombee
Afya ya
wagonjwa utuombee
Kimbilio la wakosefu utuombee
Mfariji wa wenye
uchungu utuombee
Msaada wa
wakristo utuombee
Malkia wa
Malaika utuombee
Malkia wa
Mababu utuombee
Malkia wa
Manabii utuombee
Malikia wa
Mitume utuombee
Malkia wa
Mashahidi utuombee
Malkia wa
waungama utuombee
Malkia wa
Mabikira utuombee
Malkia wa watakatifu
wote utuombee
Malkia uliyeumbwa
pasipo dhambi ya asili utuombee
Malkia uliyepalizwa
mbinguni
utuombee
Malkia wa Rozari
Takatifu
utuombee
Malkia wa Amani
utuombee
Mwanakondoo wa Mungu
uondoaye dhambi za dunia
Utusamehe Bwana
Mwanakondoo wa Mungu
uondoaye dhambi za dunia
Utusikilize Bwana
Mwanakondoo wa Mungu
uondoaye dhambi za dunia
Utuhurumie
Tuombe
Ee Bwana tunakuomba
utujalie sisi watumishi wako afya ya roho na mwili siku zote, na kwa maombezi
matakatifu ya Maria Mtakatifu Bikira daima, tuopolewe na mashaka ya sasa,
tupate nasi furaha za uzima wa milele. Tunaomba hayo kwa ajili ya Kristo Bwana
wetu. Amina.
KWA MAFUNDISHO ZAIDI UNAWEZA KUTAZAMA VIDEO HII
N:B
Lengo na madhumuni
ni kukufanya wewe mkatoliki kujifunza kusali rosary bila shida yoyote.
Imeandaliwa na Mwl. Julius Theophil
Mmbaga
Simu: 0766 500 747 Mwanza.
Maoni
Chapisha Maoni