MALAIKA MKUU MT. MICHAEL UTULINDE KATIKA VITA

 


MALAIKA MKUU MT. MICHAEL UTULINDE KATIKA VITA

Siku moja Mtakatifu Michael Malaika Mkuu alimtokea Mtumishi wa Mungu Antonia D’astonic Akamwambia kuwa “Nataka kuheshimiwa kwa sala tisa, kulingana na makundi tisa ya Malaika wa mbinguni na sala hizi ziwe Baba yetu…. X 1, Salamu Maria…. X 3

(Kwa heshima ya kila Kundi la Malaika)                                                                     

Ahadi za Mt. Mikael: yeyote atakayezoea kufanya ibada hii kwa heshima yangu, wakati wa kuelekea meza Takatifu, atasindikizwa na Malaika toka kwenye Makundi yote tisa, ambao watachaguliwa kutoka kila kundi. Zaidi ya hayo, atakayesali sala hizi tisa kila siku, ninaahidi msaada wa kudumu wa Malaika wote katika maisha yake na baada ya kifo nitamsaidia kuondolewa haraka kutoka toharani yeye na jamaa zake.

Lakini pia Mt. Michael ufurahia sana unapoweza kusali rosali yake yenye kubeba sala zote za makundi tisa ya Malaika na kwa furaha uweza kushiriki ibada hii kama alivyoweza kushiriki nami na familia yangu.

Basi kwa upendo wa Kristo nikualike kuweza kusali rosary ya Mt. Michael.

NAMNA YA KUSALI ROSARI YA MALAIKA MKUU MT. MICHAEL

Anza - ishara ya Msalaba

K. Ee Mungu nielekezee Msaada:

W. Ee Bwana nisaidie hima:

K. Atukuzwe Baba.

Kwenye chembe nne zinazofata utasali hivi kwa kila chembe.

1.    Kwa heshima ya Malaika Mkuu Mtakatifu Michael.

Baba Yetu…….

2.    Kwa heshima ya Malaika Mkuu Gabriel.

Baba Yetu….

3.    Kwa heshima ya Malaika Mkuu Raphael.

Baba Yetu…..

4.    Kwa heshima ya Malaika Mlinzi

Baba Yetu…..

Tendo la kwanza:

·         Kwa maombezi ya Mt. Michael na kweli takatifu na Malaika Serafimu, Bwana awashe mioyo mwetu moto wa mapendo kamili. Amina.

·         Baba Yetu…… x 1 Salamu Maria…. x 3.

Tendo la Pili:

·         Kwa maombezi ya Mt. Michael na kundi Takatifu la Malaika Kerubimu. Bwana atuwezeshe kuacha njia mbaya na kuenenda katika njia ya ukamilifu wa Kikiristu. Amina. Baba Yetu…… x 1 Salamu Maria…. x 3.

Tendo la Tatu:

·         Kwa maombezi ya Mt. Michael na kundi takatifu la Malaika wenye enzi Bwana atujalie roho ya unyoofu na unyenyekevu wa kweli: Amina.

·         Baba Yetu…… x 1 Salamu Maria…. x 3.

Tendo la Nne:

·         Kwa maombezi ya Mtakatifu na kundi takatifu la watawa Bwana atujalie neema ya Kushinda mahasa na tamaa mbaya. Amina.

·         Baba Yetu…… x 1 Salamu Maria…. x 3.

Tendo la Tano:

·         Kwa maombezi ya Mt. Michael na kundi takatifu la Malaika wenye nguvu: Bwana atukinge na vishawishi na mitego ya shetani. Amina.

·         Baba Yetu…… x 1 Salamu Maria…. x 3.

Tendo la Sita:

·         Kwa maombezi ya Mt. Michael na kundi takatifu la Malaika wenye mamlaka: Bwana atukinge na mwovu wala tusianguke kishawishini. Amina

·         Baba Yetu…… x 1 Salamu Maria…. x 3.

Tendo la Saba:

·         Kwa maombezi ya Mt. Michael na kundi takatifu la wakuu: Mungu atujalie roho ya utii wa kweli. Amina.

·         Baba Yetu…… x 1 Salamu Maria…. x 3.

Tendo la Nane:

·         Kwa maombezi ya Mt. Michael na ya kundi takatifu la Malaika wakuu:  Bwana atudumishe katika imani na katika kazi zote njema ili tujaliwe utukufu wa milele. Amina

·         Baba Yetu…… x 1 Salamu Maria…. x 3.

Tendo la Tisa:

·         Kwa maombezi ya Mt. Michael na kundi takatifu la Malaika: Bwana atujalie ulinzi wao hapa duniani na baadaye watuongoze kwenye furaha za mbinguni. Amina

·         Baba Yetu…… x 1 Salamu Maria…. x 3.

Ee Mtukufu Mtakatifu Michael mwana Mfalme na Mkuu wa Majeshi ya mbinguni, mlinzi wa roho, mshindaji wa pepo wabaya, Mtumishi katika nyumba ya Mungu, Mfalme na Msimamizi wetu mstajabivu mwenye nguvu za juu na akili pendevu utuokoe na maovu yote sisi tunaokutumainia. Na kwa ulinzi wako tuweze kumtumainia Mungu kila siku kwa uaminifu zaidi. Amina

K. Utuombee Ee, Mtukufu Mtakatifu Michael Mkuu wa kanisa la Yesu Kristo:

W: Ili tustahili kupata ahadi za Kristu.

Tuombe:

Ee, Mungu mwenyezi, wa milele kwa wema na huruma yako ya ajabu, umetaka watu wote waokoke, ukaweka malaika Michael kuwa mkuu wa kanisa lako. Atukinge na adui zetu wasitusumbue saa ya kufa kwetu, bali tuongozwe naye kwenye utukufu wako Mkuu, tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina.

LITANIA KWA HESHIMA YA MALAIKA MKUU MT. MICHAEL

Bwana utuhurumie,

Kristu utuhurumie

Bwana utuhurumie,

Kristu utusikie,   W. Kristu utusikilize

Baba wa Mbinguni Mungu,   W. Utuhurumie

Mwana Mkombozi wa dunia Mungu

Roho Mtakatifu Mungu

Utatu Mtakatifu Mungu mmoja,

Maria Mtakatifu: Malkia wa Malaika,   W. Utuhurumie

Mtakatifu Michael Malaika Mkuu. Nani yu sawa na Mungu   W. Utulinde na utuokoe

Mtakatifu Michael Malaika Mkuu, Shujaa mwenye nguvu na Mwaminifu wa utawala wa Mungu*

Mt. Michael Malaika Mkuu, Mtawala wa Majeshi ya Mbinguni*  W. Utulinde na utuokoe

Mt. Michael Malaika Mkuu, Shujaa aliyemshinda mkuu wa giza.

Mt. Michael Malaika Mkuu: Shujaa hodari aliyemfukuza mbinguni Lusiferi na Malaika waasi na kuwatumbukiza katika moto wa milele,

Mt. Michael Malaika Mkuu, Mkingaji wa  roho zilizoumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.

Mt. Michael Malaika Mkuu: Mlinzi wetu shujaa dhidi ya hatari zote kwa wale waliojiweka wakifu kwa Mungu*

Mt. Michael Malaika Mkuu, Mteketezaji hodari wa mafundisho ya uwongo.

Mt. Michael Malaika Mkuu: Mtetezi hodari na mlinzi shujaa wa kanisa Mama Mtakatifu.

Mt. Michael Malaika Mkuu: Shujaa aliyeharibu na kuzuia town iliyovamia Ulaya yote.

Mt. Michael Malaika Mkuu: Mshindi shujaa aliyeangusha jeshi la maharamia wasiweze kuvumia Italia ya kusini.

Mt. Michael Malaika Mkuu: Ngome imara na ya nguvu kwa wote wakuitao*  W: Utulinde na utuokoe

Mt. Michael Malaika Mkuu: Mshindi hodari wa pingamizi zote, majaribu na vishawishi vyote.

Tuombee:

Ee, Malaika wangu Mkuu, Mtakatifu Michael katika hali yangu hii ya ukosefu ninakuelekea kwa upendo mkubwa utokao moyoni mwangu. Nakuomba unisaidie mimi binafsi pamoja na wapendwa wangu wote. Saa ile ya kufa kwangu, wakati ule wa mahangaiko yetu ya mwisho utukinge na hila za shetani.

Ninakuomba na kukusihi, wewe uzifikishe sala zetu mbele ya kiti cha enzi, kwake Mungu Mkuu. Utufikishe salama nyumbani tutafurahia amani na furaha ya kweli kwa milele yote, pamoja na utukufu mtakatifu usiogawanyika, na Bikira Maria Mama wa Mungu na Mama yetu pia, aliye safi kabisa na watakatifu wote kwa milele na milele. Amina

Imeandaliwa na

Mtumishi: Julius Mmbaga

0766500747

 

 

 

 

 

 


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAHAMU JINSI YA KUOMBA SALA YA VITA

IBADA KWA MOYO MTAKATIFU WA YESU

CHANGAMOTO YA NDOTO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO

SALA KWA AJILI YA KUFUNGULIWA KUTOKA KATIKA NGUVU ZA GIZA

HISTORIA YA MAISHA YA BIKIRA MARIA