CHANGAMOTO YA NDOTO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO

 


CHANGAMOTO YA NDOTO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO

Tumsifu Yesu Kristu,

Ndugu yangu katika Makala hii napenda leo kujadili juu ya changamoto ya ndoto katika ulimwengu wa roho.

Ninaposema changamoto ya ndoto katika Ulimwengu wa roho namaanisha ni hali ya mtu kuota ndoto ambazo zinafanana sana na uhalisi wake katika hali ya kawaida, yani unaota ndoto ambayo wewe mwenyewe unaona au unahisi kabisa kitu hichi ni kweli kimefanyika, mfano wa ndoto hizi ni

1)    Unaota unakula nyama mbichi na unapohamka ukitafakari hiyo ndoto na ukigusa meno yako unawez kukuta mabaki halisi ya nyama katika kinywa chako.

 

2)    Unaota unakula kweli na ukiamka asubuhi umeshiba kabisa wala huitaji chakula chochote.

 

3)    Unaota unakimbizwa, na unakimbia kweli, ukizinduka katika ndoto unajikuta ni mtu mwenye hofu na unahema kweli na kila tukio unalikumbuka vema.

 

4)     Unaota huko katikati ya watu waliovaa nguo nyeusi au nyekundu wanakucheka au wanakula nawe.

 

5)    Unaota unafanya mapenzi na mtu usiyemjua na baada ya kuzinduka usingizini,  unajikuta kweli umechafuka kwa mbegu za kiume.

 

Ndoto hizi na zingine nyingi zinazofanana na hizi zimekuwa ni changamoto kubwa katika baadhi ya watu, na wasijue nini cha kufanya. Ili kuondokana na ndoto hizo za kutisha hebu tuangaliye baadhi ya sababu za kuota ndoto hizi.

a)    KUTOKUSALI

Watu hawa hawasali na kwa kuwa hawasali ni rahisi kushambuliwa katika Ulimwengu wa roho.

 

b)   MAAGANO

Watu wengine wanashambuliwa na Maagano ya wazazi wao katika anga la Uchawi | Ushirikina hivyo kuna mambo wanalazimishwa kuyafanya na kwa kuwa hawajui wafanye nini roho hizo zilizokuwa zinamilikiwa na wazazi wao zinaanza kuwatesa zikitaka na wao wazimiliki, hivyo wanapoota ndoto hizi za kutisha wakifaulu kwenda kwa waganga wa kienyeji, Mganga huyo anawapa maelekezo maana ulimwengu wao ni huo huo na mtu huyo anajikuta naye anaendekeza Maagano ya wazazi wake bila kujua au kwa kujua.

 

c)    USHIRIKINA

Unapokuwa Mshirikina, wewe mwenyewe unafungua mlango wa maadui zako kukushambulia katika ndoto, hivyo waovu wenzako ni rahisi sana kukubeba na kukufanya wanavyotaka.

 

d)   KUTOTAMBIKIA

Baadhi ya watu wameacha kutambikia na hata watoto wao waliozaa mijini nao hawajui kabisa mitambiko, kwa kuwa katika ukoo huo kuna roho zilizoalikwa toka enzi ya Mababu kuishi katika ukoo huo na zilikuwa zinatolewa sadaka, inafika mahali zinahitaji kutambuliwa na wahusika, na hivyo huja katika ndoto kwa hasira na kwa kuwa watu hatusali, hupata nafasi kubwa kututesa.

 

MATOKEO YA BAADHI YA NDOTO HIZI KATIKA ULIMWENGU

WA MWILI

 

A.   UGUMBA | KUTOOLEWA

Msichana anayeota kujamiana katika ndoto anaweza kukumbana na changamoto zifuatazo.

 

·         UGUMBA

Hizi roho zinaweza kumfunga kizazi asizae kabisa au kuota ana mimba na kuzaa mtoto katika Ulimwengu wa roho au kujikuta ananyonyesha usiku akiwa kalala, wakati huo hana mtoto.

 

 

·         KUTOOLEWA

Kwa kuwa usiku anaota kujamiana, katika Ulimwengu war oho mtu huyo anamilikiwa na roho hiyo ambayo nayo haitaki kuchangia mme, hivyo kila Wanaume wakija kumposa Binti, roho zilizo mmiliki binti huyo, zinawafukuza na wakitoka hapo uchumba umekufa kabisa. Mwanaume huyo harudi tena.

 

·         UCHAWI

Baadhi ya watoto au watu wazima wamejikuta wamejifunza uchawi katika ndoto, usiku akiwa amelala nafsi yake inaondoka na kwenda kufundishwa Uchawi zoezi ili likikamilika haijalishi ni miaka mingapi, nafsi ile ya mhusika hurudishwa katika mwili wake na hapo mtoto au mtu huyo uonyesha uchawi wake halisi kwa vitendo, yawezekana hata ndugu zake wakashangaa ndugu yao huo uchawi katoa wapi, kumbe alifundishwa katika ndoto.

 

·         MAGONJWA

Kuna magonjwa mengine ni matokeo ya ndoto, mfano mtu anaota analishwa vitu vibaya na akiamka ni mgonjwa kweli wa tumbo n.k

TIBA YA UHAKIKA WA NDOTO HIZI

Ndugu yangu katika Kristo, tiba pekee ya ndoto hizi ni sala, Sali sala ya kufunguliwa kutoka katika nguvu za giza. Sala hii ambayo himo humu ndani. Itafute na kuanza kuisali bila kuchoka, sala hii itakutenga mbali na ndoto zote mbaya yaani hautoota tena.

CHANGAMOTO YA SALA HII YA KUFUNGULIWA KUTOKA KATIKA NGUVU ZA GIZA

Ø  Kama una nguvu za giza unahitaji msaada wa kusali sala hii maana wewe Mwenyewe hautaweza, nguvu hiyo itakuthibiti kusali na kujikuta wakati wa sala unalala kabisa au kuzimia.

 

Ø  Unaposali sala hii unaweza kulipuka mapepo hivyo kama mpo zaidi ya mmoja wengine wataendelea kusali tu mpaka hali hiyo itakapokutoka, kwa kusali hivyo hivyo kila siku, kamwe hauwezi kuota ndoto hizo.

 

MWISHO

Dumu katika sala katika Maisha yako yote na Mungu atakubariki sana.

 

Imeandaliwa na Mtumishi: Julius Mmbaga (0766500747)

 


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAHAMU JINSI YA KUOMBA SALA YA VITA

IBADA KWA MOYO MTAKATIFU WA YESU

MALAIKA MKUU MT. MICHAEL UTULINDE KATIKA VITA

SALA KWA AJILI YA KUFUNGULIWA KUTOKA KATIKA NGUVU ZA GIZA

HISTORIA YA MAISHA YA BIKIRA MARIA