UPAGANI ULIOJIFICHA KATIKA MWAMVULI WA DINI
Ndugu
zangu wapendwa katika Kristo. Naomba leo kwa pamoja tutafakari huu upagani
uliojificha katika mwavuli wa dini.
Upagani
kwanza ni nini? Mimi naweza kusema upagani ni ile hali ya kuishi bila kujua
uwepo wa Mungu, ni hali ya kuishi katika imani isiyofungamana na Mungu
mwenyezi, ni hali ya kutegemea miungu wengine, kutomjua Mungu kabisa.
Ndugu
zangu baada ya kujaribu kuelezea upagani kwa tafsiri yangu, hebu tujiulize tena
dini ni nini? Dini ni mkusanyiko wa watu wenye imani moja wanaokusanyika pamoja
kwa lengo la kumwabudu Mungu wao, kusali na kuomba pamoja, kuna dini za aina
nyingi lakini zote zinakusanyika pamoja kwa imani yao kuongea na Baba yetu
aliye mbinguni, na dini uanzia ndani ya familia.
Watu
wenye dini ujitenga kabisa na mambo ya kipagani utembea na Mungu Muumba nchi na
vitu vyote vinavyoonekana na wakiamini Mungu wao anaweza kila kitu, Mungu wao
anajitosheleza wala haitaji msaada wowote, hivyo watu wenye dini yaani wenye
kuamini uwepo wa Mungu mmoja, daima wakipata changamoto, shida yeyote upiga
magoti na kuomba msaada kwa Mungu wao, na Mungu wao ambaye ni Baba yetu aliye
mbinguni uwajibu maombi yao, kupitia kwa mwanaye mpendwa Bwana wetu Yesu Kristo.
Watu
wenye dini hawafanyi kafara, maana kafara yao ya mwisho ni mwili, damu, roho ya
Bwana yetu Yesu Kristo aliyejitoa msalabani kwa ajili ya ukombozi wao. Watu
wenye dini uamini kila kitu kinachofanyika ni mapenzi ya Mungu na daima umpa
Mungu utukufu, hata kama wanapitia mateso, maangaiko daima uwomba, umtegemea
Mungu wao wala hawaabudu katika madhabau yeyote zaidi ya ile ya Mungu wao aliye
hai.
Laikini
katika watu hawa wenye dini ndani yao kuna mchanganyiko wa wapagani, yaani watu
wanaoigiza kwamba Mungu yupo, lakini hawamwamini huyo Mungu kama anaweza
kutatua matatizo yao, hawa ni watu wanaopenda kupitia njia fupi ili kupata
ufumbuzi wa matatizo yao, hawa ni watu washirikina, wachawi, ni watu wenye
kuhudumu katika madhabau ya shetani, ni watu wenye kumtii sana shetani kuliko
Mungu, ni watu wenye kiburi cha kuzimu ambacho wanakificha katika mwamvuli wa
dini, watu hawa ukiwaona Makanisani ni wanyenyekevu, wengine ni viongozi, ni wa
kwanza kanisani, lakini ukichunguza matendo yao, yanaweza kukufanya nawe kufa
moyo hata kwenda kusali. Lakini tukumbuke watu wote ni wa Mungu, wawe wapagani,
wawe wanadini wote hawa Mungu uwapenda na kuwatendea mema kadri ya mapenzi
yake, yaani daima Mungu utimiza mapenzi yake kwetu, changamoto ni kwetu
kutimiza mapenzi ya Mungu.
Hivyo
tunashuhudia watu hawa ambao leo nawaita ni wapagani maana licha ya kujiita
kuwa wanadini, lakini hawatendi yale yawapasayo kutenda wawapo
mafichoni/gizani, wanatenda sawa sawa na giza wanafukuza nuru kabisa, watu hawa
wamevaa upagani ambao wanauficha ndani ya dini. Maana wanafanya mabo ya
kipagani ambayo hayanatofauti na yule asiye mjua Mungu, wanafanya kinyume na
amri za Mungu. Hebu tuangaliye watu hawa baadhi ya mambo ya kipagani
wanayofanya ili ujue au yawezekana nawe ukawa ni mmoja wapo ili ujifunze na
uyaache kabisa na kutembea na Mungu tu, ndani ya dini yako, hapa tunajumuisha
mambo yote ya kishirikina – maana yote hayo ni upagani tupu.
1. Kuacha kumtegemea Mungu na kuabudu mapepo, majini n.k
huku kila siku ya kuabudu unakwenda kanisani huo ni upagani.
2. Kufanya kafara au kutambika kwa kutoa sadaka kwa
mashetani ili yakulinde, yakusaidiye, yakupe utajiri n.k huo ni upagani.
3. Kuzindika nyumba au mji kwa kuweka ulinzi wa kipepo
ukiamini Mungu hawezi kabisa. Huu ni nao ni upagani.
4. Kukata kata mwili wako na kuutoa damu kwa kutumia wembe
au kisu kisa kujipakaa dawa nyeusi au rangi yeyote eti ni ulinzi na unakwenda
kanisani kusali, huo ni upagani ndani ya dini.
5. Kuzaa mtoto na kumfanyia matambiko mbalimbali mpaka juu
ya jina lake huo ni upagani, badala ya mtoto kumpeleka kanisani na kubarikiwa,
kumkabidhi mikononi mwa Bwana, wewe unaanza kumkabidhi mtoto wako kwa shetani
huo sio Ukristo ndugu yangu ni upagani.
Mambo
yote wewe unayejiita wa Kristo, unakwenda kanisani na Biblia yako, na unafanya
mambo yanayofanana na hayo, wewe ni mpagani uliojificha katika mwamvuli wa
dini, ukiwa kanisani ni wakwanza kuimba mapambio, huku ukisema Mimi ni
Mkatoliki, Mimi ni Mlokole, Mimi ni Msabato, Mimi ni Mlutheri, Ndugu yangu
shetani haogopi dini yako, shetani anaogopa imani yako thabithi katika dini
yako, na wala wewe kuwa Mlokole au dini yoyote sio kibali cha wewe kwenda
mbinguni, Mungu anaona matendo yako, Imani yako, hivyo kutuigizia sisi wanadamu
ambao hatuji matendo yako unayoyafanya ufichoni, matendo ya kipagani, Mungu
anakuona, kuvaa mwamvuli wa dini mbele yetu ni maficho ya muda mfupi sana maana
Mungu anakuona, siku ile ikifika utasema, Mimi nilikuwa Mchungaji, nilikuwa
Sister, Nilikuwa Padri, nilikuwa Mwamini mzuri kabisa na nilikutumikia, ndipo
hapo matendo yako yote yataonekana wazi maana Mungu wetu ni Mungu wa haki kamwe
haoneii mtu na huruma yake haina mipaka, atakuonyesha matendo yako yote na
utapokea hukumu yako sawa sawa na haki yako.
Hivyo
niitimishe kwa kusema wewe ambaye unamdanganya Mungu, jua unajidanganya
mwenyewe, usitudanganye sisi ambaye hatukujui vema, tunakushangilia na kukupa
cheo ndani ya kanisa kumbe wewe ni Mchawi, yote unayofanya katika Mwamvuli wa
dini yako yana mwisho wake.
Mungu
atubariki sana.
Imeandaliwa
na:
Mtumishi, Julius Mmbaga
0766500747
Maoni
Chapisha Maoni