SIKUKUU YA KUMKUMBUKA MAMA BIKRA MARIA KILA TAREHE 01 JANUARY

 


Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu
Kanisa katoliki lina mafundisho makuu manne kuhusu mama Bikira Maria, yaliyotayarishwa na kutolewa na  mababa wa Kanisa,  baada ya kusoma na kutafiti mengi kuhusu maisha ya Mama Maria.

Lakini hata maandiko matakatifu (Luka 1:26-38) tunaona jinsi Malaika Gabrieli alivyotumwa na kumpasha habari kuhusu kuzaliwa kwa Bwana Yesu Kristo. Na tuliona jinsi alivyopokea habari hizo kwa unyenyekevu.  Hapo ndipo nafasi yake kama mama wa Mungu inapoonekana .Uthibitisho zaidi ulipatikana tena katika Luka 1:42-43,  na kutiliwa mkazo katika Wagalatia 4:4.(Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria)

Hivyo basi, mwaka 1944, Baba mtakatifu Pius X11, aliiweka rasmi siku ya tarehe 1 Januari, kama Sikukuu ya kumkumbuka Mama yetu Bikira Maria, kuwa pia ni Mama wa Mungu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI YA KUSALI ROSARI TAKATIFU YA BIKRA MARIA

ROZARI YA KUWAOMBEA MAREHEMU TOHARANI

MALAIKA MKUU MT. MICHAEL UTULINDE KATIKA VITA

IBADA KWA MOYO MTAKATIFU WA YESU

TAMBUA UMUHIMU WA KUOMBEA MIMBA KWA MAMA MJAMZITO

CHANGAMOTO YA NDOTO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO