MKAKATI WA WACHAWI KUKUZA NA KUENEZA UCHAWI
MKAKATI WA WACHAWI KUKUZA NA KUENEZA
UCHAWI
Tumsifu Yesu Kristo.
Ndugu
zangu katika Kristu, Katika makala hii napenda kuwashirikisha mkakati wa kukuza
na kueneza uchawi.
Unaweza
usielewe, lakini tunakoelekea tutegemee kuwa na wachawi wengi zaidi, kwa sababu
wachawi wamegundua njia bora na nzuri ya kueneza uchawi wao ni kuwafundisha
watoto wadogo, na kuwalisha viapo katika Ulimwengu wa giza kiasi kwamba hata
mtoto akijitambua anashindwa kujitoa kabisa.
1. Watoto wa wachawi wenyewe
2. Watoto Yatima
3. Watoto ambao wazazi wao wanamafarakano
4. Watoto ambao ndugu zao ni wachawi
5. Watoto ambao marafiki na majirani zao ni wachawi na ni
rafiki wa familia zao. (kuozeshana watoto wao kwa wao kwa lengo la kukuza
uchawi wao.)
·
Watoto hawa huibiwa
nafsi zao, na nafsi zao hizo upelekwa kufundishwa uchawi kwa muda mrefu, na
mtoto aliyeibiwa nafsi akilala usiku uota mambo mazito akifanya ikiwa ni pamoja
na kunywa damu, kula nyama mbichi, kushiriki vikao na watu waliovaa nguo
nyekundu au nyeusi, katika hali hiyo atafundishwa mambo mengi katika ulimwengu
wa roho kwa kutumia nafsi yake, na hakiisha komaa nafsi ile uachiwa kurudi
katika mwili wake ikiwa na uzoefu wa hali ya juu, hapo hapo mtu huyu uanza
kutenda kwa uhalisia wake matendo ya kichawi, kuchezea wenzake kwa nguvu za
giza n.k na katika hali yote atakuwa ni mwenye furaha.
Kitendo
cha wachawi pia kuozeshana watoto wao ni mkakati wa kukuza na kurisisha uchawi
wao kizazi hadi kizazi bila shida yeyote.
·
Watoto yatima pia
wanapata changamoto hii kwa sababu wachawi wanatambua wazi kuwa mtoto huyu sio
rahisi kupata msaada wa kiroho hivyo, ni rahisi wao kumtumia watakavyo, na
mtoto huyu uweza kukataa shule kabisa kama anasoma, na hapo uweza kuota mambo
makubwa kumbe anafundishwa na akikomaa uona raha na kuendelea na kazi yake ya
uchawi.
Tatizo
kubwa linalosababisha ongezeko la uchawi pia ni familia nyingi hazisali, na
familia nyingi uamini na kutegemea nguvu za giza.
·
Ndugu zangu kazi ya
Mchawi ni kuharibu na furaha ya mchawi ni kukuona wewe unateseka, kwa lugha
fupi, mtu yeyote anayefurahia wewe unavyoteseka mtu huyo ni mchawi wako, kwa
sababu angeweza kukufanya wewe uteseke angefanya ila kwa kuwa awezi na sasa
anafurahi mateso yako huyo hana tofauti yeyote na mchawi tu.
·
Ukitaka kujua uchawi
unaongezeka unaweza kufanya utafiti kwa watoto wa darasa la chekechea, la
kwanza na la pili, watoto hawa ukijiusisha na kuwa rafiki yao mwema na kuongea
nao kwa akili utaona watoto wenye kutoka familia za kichawi, yaani watoto walio
wachawi watakavyo kusimlia mambo ya nyumbani kwao kwa raha kubwa, jinsi
anavyologa yeye na Bibi yake au Babu yake historia zingine unaweza cheka
kidogo.
Lakini
ndivyo ilivyo. Hawa watoto ndio tunategemea kuwa viongozi wetu wa baadaye maana
baadhi ya wachawi hujua umuhimu wa elimu lakini wengine hawajui kabisa na hao
ni wengi, ukikuta mchawi mwenye kupenda elimu atawaongozea darasani na walimu
walio wachawi wote watampenda sana, hivyo tutegemee kwa stahili hii kupata
viongozi wachawi au washirikina mno. Ili kuzuia ongezeko la uchawi tufanyeje?
Ø Tunatakiwa kuwalea watoto wetu kwa kuwaelekeza ili
wamjue Mungu, wampende, watenge muda wa kuongea naye.
Ø Kuwaombea watoto wetu kwa kuwatenganisha na maagano yote
toka mti wa familia ili yasiweze kuwasumbua katika makuzi yao.
Ø Kuzifanya nyumba zetu kuwa kanisa dogo, yaani kusali
bila kuchoka ndani ya familia.
Ø Kuongea na watoto wetu, kuna watoto wanateseka sana,
wanashindwa wamshirikishe nani ili kupata msaada. Tutenge muda wa kuongea na
watoto hawa na kuwashirikisha upendo wa Mungu.
Hebu tujiulize
swali, je mchawi pia husali?
Jibu ni ndiyo, wachawi walio wajanja uigiza kusali, na nikwanza
kanisani, upenda kujionyesha sana kuwa wao ni wacha Mungu sana, kwenye vikundi
vya sala wapo, lakini uchagua vikundi, vile vilivyo dhaifu ujiunga navyo.
Wachawi wa namna hii ni rahisi sana kuwakomboa maana wanapenda kusali wakiwa na
mikoba yao, ikitokea siku wakakutana na nguvu ya Mungu ukombolewa kabisa.
Ndugu zangu katika Kristu, tuache ushirikina, Tusali na
tuwafundishe watoto wetu kumjua, kumpenda Mungu na kumtumikia, kwa kufanya hivi
tutapunguza sana, ongezeko la wachawi ndani ya koo zetu.
Mungu atubariki
sana.
Unaweza kutazama video hizi ili kuzama ni mbinu gani Wachawi utumia kwa watoto ili kueneza uchawi wao.
Tazama binti huyu aliyeandaliwa kuwa Mchawi.
SHEMU YA PILI YA VIDEO YA BINTI ALIYEANDALIWA KUWA MCHAWI.
SHEMU YA TATU YA VIDEO YA BINTI ALIYEANDALIWA KUWA MCHAWI.
Maoni
Chapisha Maoni