MADHARA YA VIONGOZI WASHIRIKINA
MADHARA YA VIONGOZI WASHIRIKINA
Tumsifu Yesu Kristo.
Ndugu
zangu wote tunajua maana ya madhara, madhara ni uharibifu au athari mbaya
tunaweza kuziona baada ya kufanya kitu Fulani na ushirikina ni wazo ambalo
halina sababu yenye msingi katika maarifa au mang’amuzi na neno ili hutumiwa
kwa kutaja imani ambazo hazina msingi au tunaweza kusema ushirikina ni sayansi
iliyotolewa kwa uhusiano kati ya viumbe visivyo hai na wanadamu, uchawi na
ushirikina yanaweza kufanana, ushirikina ni kitendo cha kwenda kutafuta msaada
wa kiroho au kimwili katika Mamlaka ya giza, namaanisha kwa shetani na mapepo,
majini yake yanayofanya kazi kupitia watu wanaoitwa waganga au wachawi.
Hivyo
leo tuangalie watu hawa ambao ni viongozi wetu na niwashirikina yaani katika
utendaji wao wa kazi wanawategemea waganga au wachawi, watu wa namna hii
hawawezi kuleta maendeleo katika eneo lao la kazi kwa sababu ya tumia nguvu za
giza zaidi wanaweza kusababisha mambo yafuatayo katika maeneo yao ya kazi:-
1.
MIGOGORO
Tukumbuke washirikina ni watu wanaofanya kazi zao au
kutimiza wajibu wao kwa kutumia nguvu za giza ambazo zimetengenezwa katika
maumbo mbalimbali kama vile pete, irizi, cheni n.k au manuizo, kazi zote hizi
usimamiwa na mapepo hivyo kama wewe ni mtu wa sala sana, watu hawa mtapambana
nao na watakuchukia sana na kutengeneza migogoro isiyo ya lazima.
2.
MAENDELEO
Viongozi wa namna hii hawawezi kuleta maendeleo hata
mara moja katika kipindi chao chote cha utawala, maana wanaamini wapo hapo kwa
msaada wa nguvu za giza na ni watu hatari sana, wasio na utu hata kidogo maana
wanaongozwa na mapepo, au wanaamini ulinzi wa nguvu za giza.
3.
KUSALI
Ni watu ambao hawapendi kusali kabisa au kushiriki
matukio ya kiibada, hata ruhusa zao ni shida, na wanapenda sana kutukuzwa,
kuheshimiwa hata pasipo stahili heshima.
4.
KUONGELEA NGUVU ZA GIZA
Watu hawa hawapendi kabisa kusikia mjadala wa kulaani
nguvu za giza, zaidi utasikia wakisisitiza hakuna ushirikina, hakuna uchawi na
hata sala zao ni za kujionyesha kuwa wanasali sana, kuficha uovu wao lakini
nyuma ya pazia ni washirikina wa ajabu.
5.
USHAURI WAO
Ushauri wao unategemea na
wewe ulivyo, ukiwa ni mtu wa dini, kama ni boss wako atajifanya kukushauri sawa
sawa na ulekeo wako kuwa umtegemee Mungu, kama ni mshirika mwenzake atakuongoza
kwa mtaalamu mwingine zaidi.
6.
MAHUSIANO SEHEMU YA KAZI
Kiongozi mshirikina uimarisha mahusiano makubwa na
washirikina wenzake, wachawi wenzake kwa kila jambo. Awawapendi kabisa watu
wanaosalisali, na wanateteana sana katika maeneo ya kazi hata boss akija na
wazo la kipuuzi, wazo hili litapita kwa asilimia zote, sio wa kweli.
7.
MWISHO WAO.
Viongozi wa namna hii hawamalizi vizuri uongozi wao au
maisha yao, maana kwa ujeuri wao watakuwa wameathiri watu wengi katika uongozi
wao kwa kuwanyanyasa, hivyo wengine upata malipo yao hapa hapa.
HATUA ZA KUCHUKUA
KUPAMBANA NA VIONGOZI WASHIRIKINA
·
Kumbuka kuwa wewe ni
mwanadamu uliumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, kumbuka pia kuwa umepewa mamlaka
na Mungu ya kutawala viumbe vyote na kuvitiisha, kumbuka pia mapepo, majini na
nguvu zingine zote za kichawi zipo chini ya mamlaka yako kwa jina la Yesu.
·
Vaa silaa zote za vita kama ilivyoandikwa Waefeso 6:10-20, tumia mamlaka hayo kumfunga boss wako
Mshirikina, sambaratisha na nguvu yake yote aliyoweka kwenye Ofisi yake au
anayotembea nayo, ukorofi wake wote mbele yako ushughulikiye kwa nguvu ya
maombi, akikufokea wala usiangaike kumjibu kimwili bali mjibu kiroho, funga
hiyo roho inayokuchukia kwa jina la Yesu, hata mkianza kikao kitawale kikao
hicho kwa kusema kwa Imani kuu, (Nakifunga kikao hiki kwa jina la Yesu mwovu
yeyote hana Mamlaka nacho) jitahidi uwe mtu wa sala daima, na hapa utaona
kiongozi wake anabadilika ghafla na kukupenda, lakini pia kutenda haki na
kuleta maendeleo lakini ikishindikana kuwa hivyo inakuwa kinyume chake kwa
maana anaweza kufukuzwa kazi, kushushwa cheo au kuhamishwa eneo ulipo na mambo
yote haya yanatokea automatic yaani kwa mapenzi ya Mungu.
·
Viongozi hawa upenda
sifa sana hata wasizositahili wewe msifu tu, mtapatana, wala usijenge nao
mazoea hadi kwenye familia yako, wanawivu sana wa maendeleo, kuwazoesha
nyumbani au kuwasimlia maendeleo yako ni hatari sana, hivyo acha kuwasimlia
maendeleo yako.
Mwisho na muhimu dumu katika sala,
wataomba uhamisho wenyewe au kujihudhuru nafasi zao na wewe daima ndio mshindi.
Maoni
Chapisha Maoni