IJUE NGUVU YA MSAMAHA
IJUE NGUVU YA MSAMAHA TOKA MAKALA HII ILIYOANDALIWA
NA MTUMISHI JULIUS MMBAGA
Ndugu
Msomaji leo nataka ujue nguvu ya msahama katika kufanikiwa katika safari ya
maisha yako.
Sisi
kama Wakristo tumekuwa kukisali sala ya Baba Yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe,
ufalme wako ufike utakalo lifanyike duniani kama mbinguni, utupe leo mkate wetu
wa kila siku, utusamehe makosa yetu kama tunavyo wasamehe na sisi waliotukosea,
usitutie katika vishawishi bali utuokoe maovuni. Amina.
Salah
hii ya Baba yetu tunaisali sana., je ni kweli tunawasamehe wenzetu waliotukosea
hebu soma Mt. 6-7-15 na ni vema uelewe wazi kuwa :-
1. Tunafurahia msamaha wa Mungu kwa kiwango kile ambacho
sisi pia tupo tayari kuwasamehe wengine.
2. Hivyo kila mtu ambaye hujamsamehe maishani mwako ni ushahidi
wa kuwepo kwa dhambi zako katika maisha yako ambazo Mungu hajasamehe.
3. Kutosamehe ni kitu kigumu sana lakini ni chenye madhara
kwa sasa na baadaye, baadhi ya watu wanaugua magonjwa ambayo tiba yake ni
kusamehe tu, unakutana na mtu anaugonjwa wa shinikizo la damu, ana ugonjwa wa
hasira na kila siku anapanga kulipiza kisasi, anatamani kujiua au kuuwa,
anatamani kusababisha madhara makubwa, kwa sababu tu ameshindwa kusamehe, mpaka
anakuwa na magonjwa kwasababu ya ugumu wa moyo wake, na hii inasababisha roho
chafu, roho za kiburi, roho za kisasi.
Siku
moja nilikuwa natoa huduma, na baada ya huduma nilimsihi aliyekuwa mgonjwa
kuwasamehe watesi wake, naye alikataa kabisa, baada ya ushauri wa kutosha
alikubali kuachia msamaha, basi alipofumbua kinywa chake kutangaza msamaha,
aliruka juu na kudondoka chini na kuviringika kama tairi la gari na mwisho
alinyooka na kupiga kelele na hapo akaweza kuachia msamaha na kupona kabisa, na
ile nguvu kwa nguvu ya msamaha ilitoweka kabisa na alijisikia mwili mwepesi.
4. Hebu tujitafakari
sote sisi kama wakristo usipokubali kusamehe ni dhahiri nawe hautaki kusamehewa
dhambi zako, na usiposamehewa dhambi zako, utaurithije uzima wa milele maana hakuna
kinyoge kitaingia kule.
5. Kama uwezi kusamehe ni muhimu kwamba neema ya kusamehe
kila unaposimama kusali, kama una neno na mtu msamehe na wewe usamehewe maana
usiposamehe hata maombi yako hayatasikilizwa na Mungu hebu soma Mark 11:25-26
inasema hivi (Mnaposimama kusali, msameheni kila mtu aliyewakosea chochote, ili
Baba yenu aliye mbinguni awasamehe nyinyi makosa yenu) hivyo kama utaamua
kukomaa na kutosamehe watu makosa yao basi ujue hata wewe hautasamehewa na
usiposamehewa huwezi kusikilizwa maana Mungu hayasikilizi maombi ya mwenye
dhambi soma Yohana 9:31 (Twajua kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi, bali mtu
akiwa ni mcha Mungu na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo) Zaburi 66:18
(Kama ningelinua maovu moyoni mwenyezi Mungu hangalinisikiliza)
6. Nguvu ya kusamehe tunakuwa nayo katika somo la utoaji
ukisoma Mathayo 5:23 -26 (Patana na mshitaki wako upesi mkiwa bado njiani
kwenda mahakamani. La sivyo, Mshitaki wako atakukabidhi kwa hakimu, naye hakimu
atakukabidhi kwa Askari, nawe utafungwa gerezani, kusamehe pia ni chanzo cha
kiburi, wewe unakuwa na kiburi cha kuomba msamaha kwa jambo dogo, ambalo
lingemalizika kwa mazungumzo tu, lakini kiburi na hatimaye ukifikishwa mahakama
sharia uchukua mkondo wake na hatimaye waweza kufungwa kabisa.
7. Watu wengi wanasali, wanamuomba Mungu usiku na mchana
moambi yao, kumbe Mungu amekwisha wajibu maombi yao, na maombi yao yako hewani
yanazunguka zunguka tu, kwa sababu haya pa kuingia, mioyo yao imejaha visasi,
mioyo yao imejaa kutosamehe, imejaa mahangaiko wabaki kulalamika Mungu
hawasikii wakiomba na hatimaye wanakuwa washirikina hodari maana huko na
kutosamehe kwao vinapatana kabisa.
8. Tukumbuke kabisa kutosamehe kwako kunaathiri mpaka
utoaji wako wa sadaka kwa Mungu soma Luka 17:3-4 (Jihadhari kama ndugu yako
akikukosea, muonye, akitubu msamehe na akikukosea mara saba kwa sikou na kila
mara akirudi kwako akisema, nimetubu, lazima umsamehe) Hivyo unaweza kuona neno la Mungu
linasisitiza kusamehe maana ushindi wa maombi yako na mafanikio yako huko hapo,
yatupasa tujilinde ili kule kukosewa kwetu kusiwe sababu ya kuyaharibu kabisa
maisha yetu, tuombane msamaha tuache kiburi.
Kusamehe hakuna ukomo, Mathayo 18:21-22 (Kisha Petro
akamwendea Yesu, Je, ndugu yangu akinikosea nimsamehe mara ngapi? Mara saba? Yesu akamjibu, "sisemi mara
saba tu, bali sabini mara saba) Utaona hesabu hii kwa elimu ya Petro ilikuwa
hesabu kubwa mno hii inatupasa kutambua wazi kusamehe hakuna ukomo na kusamehe
sio kuwa mjinga.
Mateso mengi ambayo watu wanapitia maishani kwa sababu
hawapo tayari kusamehe, kutosamehe kunatoa nguvu kwa watesaji wako na hapa
tusome Mathayo 18:32-35 (Hapo yule bwana alimuita huyo mtumishi akamwambia,
wewe ni mtumishi mbaya sana! Uliniomba, name nikakusamehe deni lako lote, Je,
haikukupasa nawe kumhurumia mtumishi mwenzako kama nilivyo kuhurumia? Basi,
huyo Bwana alikasirika sana, akamtoa huyo mtumishi aadhibiwe mpaka hapo
atakapolipa deni lote, na Baba yangu aliyeko mbinguni atawafanyieni hivyo hivyo
kama kila mmoja wenu hatomsamehe ndugu yake kwa moyo wake wote.
Hapo tunaona Yesu amekuwa wazi mno na kutuonyesha
madhara ya kutosamehe, Ndugu yangu sisi tuliosamehewa na Bwana nasi tusamehe na
katika kusamehe tunapokea neema kubwa sana na maombi yetu yanajibiwa, hebu
tukasome
Efeso 4:31-32, Wakolosai 3:12-13
Warumi 12: 7-21 (Msimlipe mtu ovu kwa ovu) ushindeni
ubaya kwa wema.
Ndugu zangu hata kama una hasira Efeso 4:26-27 inasema
Muwe na hasira ila msitende dhambi, jua lisichwe na uchungu bado haujawatoka
wala msimpe Ibilisi nafasi.
Mungu atubariki na kutujalia neema ya kusamehe katika
maisha yetu.
Imeandaliwa na
Mtumishi: Julius Mmbaga
0766500747
Maoni
Chapisha Maoni