ELIMU NA NGUVU ZA GIZA
ELIMU NA NGUVU ZA GIZA
Tumsifu Yesu Kristo
Ndugu zangu wapendwa katika Kristo Yesu, leo napenda kuwashirikisha changamoto
kubwa ambayo inawapata baadhi ya watoto katika elimu nasi tunaona ni kitu cha
kawaida tu.
1. Mtoto kukataa shule kabisa bila sababu za msingi.
Tumeona baadhi ya watoto wengine wanakataa shule kabisa
hasa wakati wanapoelekea madarasa ya mitihani au kukaribia madarasa ya
mitihani, na hali hiyo inaonekana katika jamii kama kitu cha kawaida, nakusema
mtoto huyu kakataa shule. Hapana, baadhi ya watoto wanasongwa na nguvu za giza
na kujikuta hawataki shule kabisa na hatimaye uacha kabisa masomo. Na hata
akiacha shule hawezi kufanya kitu chochote cha maana kwa sababu nguvu iliyopo
ndani yake bado inamdhibiti na kukamata mafanikio yake. Mtoto wa hivi akikutana
na nguvu ya Mungu atapenda shule na kurudi darasani na kuendelea na masomo kama
kawaida.
2. Mtoto kuugua macho hasa wakati wa mitihani
Kuna watoto wanapata shida kubwa ya macho hasa
wanapoingia madarasa ya mitihani na akitoka darasa hili maana yake akilivuka
darasa hilo na macho yake upona kabisa, anaweza kuhisi kama mchanga kwenye
macho, macho huvuta kila anaposoma, hatimaye huwa mzembe kusoma au kujisomea na
kusababisha kufeli au wakati wa mitihani haoni maswali kabisa. Mfano halisi
siku moja jioni alikuja binti wa kidato cha pili nyumbani kwangu jioni na mzazi
wake, na kesi yake kubwa ni tatizo lililomkumba katika chumba cha mtihani
akadai alipogawiwa mtihani wake haukua na maswali na hata alipobadilishwa, hakuweza
kuona maswali yeyote kwa mitihani yote miwili na bado mitihani ilikuwa
inaendelea ya kidato cha pili.
Binti huyu nilimuomba tusali naye pamoja na baada ya
kusali, nguvu ya kichawi ililipuka ndani yake na kudai hawataki haendelee na
masomo, lakini baada ya maombi ilimtoka na kesho yake aliweza kuona mitihani
yake yote vizuri na kuifanya vema.
3. Mtoto kupata zero au kufeli kabisa.
Kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya watoto wenye akili
nje ya darasa, lakini wanapoingia ndani ya darasa hufanya vibaya sana katika
masomo yao, hata mkimtazama kwa kumpa mazoezi ya kawaida nje ya darasa unaweza
kujiuliza maswali ya kwanini mtoto huyu anapata zero na usipate majibu yake.
Kumbe anakamatwa ufahamu wake katika mitihani na nguvu ya giza ndiyo sababu
anafeli, kuna roho inamvaa wakati wa mitihani na kumfanyia mitihani hiyo, hivyo
hivyo na kwa kuwa familia nayo haina tabia ya kusali, mtoto huyu ataonekana
mjinga na hawezi kuendelea na shule tena, hivyo safari yake ya elimu hukomea
hapo hapo. Nitatoa mfano kwa watoto wawili mapacha, watoto hawa walikuwa ni
mapacha wa kike na wa kiume na wazazi wao wote ni waalimu, watoto hawa
walionekana kufanya vibaya sana darasani licha ya juhudi zote za waalimu wao na
wazazi wao na viboko vya kutosha bado wote walikuwa wa mwisho darasani kwa
kufuatana, walipoingia darasa la saba, wazazi kwakujua uwezo wao waliwarudisha
darasa la tano na kuwapeleka private school, bado huko walikuwa wa mwisho
darasani. Basi wazazi walipoingia kwenye maombi, watoto wale wote walikombolewa
akili zao na mmoja kati yao alikuwa mateka kuzimu kwa miaka nane, hivyo watoto
hawa walikombolewa wakiwa tena wamefika darasa la sita kuelekea la saba,
walipambana kusoma kwa bidii na walifanya vizuri katika elimu yao, mpaka ninapoandika makala hii wakike yuko chuo
mwaka wa pili na wakiume anaingia kidato cha sita na wote wako huru na
wanaendelea vema kabisa na masomo yao.
4. Mtoto kuumwa kichwa kwa maumivu makali sana.
Kuna watoto wamekuwa wakiugua sana na hasa kichwa
wapoingia madarasa ya mitihani au wanaingia kwenye chumba cha mitihani,
wakitoka kwenye chumba cha mitihani wanapona
au wakivuka darasa la mitihani wanapona kabisa, mtoto wa namna hii
anahitaji msaada wa maombi ili nguvu inayoweka makao katika kichwa chake
imwacha huru kabisa ili aweze kuendelea
na masomo yake vema kabisa, na kama familia inasali kweli inaweza kumsaidia
vema.
5. Kuugua ugua wakati wa mitihani.
Baadhi ya watoto wakati wa mitihani ndio muda wake wa
kuuguaugua, kila leo yuko hosiptali, wengine inafikia hatua ya kuhairisha
kufanya mitihani kwa sababu ya ugonjwa, kila inapokaribia mitihani ni mgonjwa,
mitihani ikipita hupona kabisa, na hatimaye kutokana na changamoto hiyo mtoto
huacha shule nasi wazazi huona kuwa ni poa tu.
6. Kusinzia darasani wakati mwalimu anafundisha
Baadhi ya watoto wanatabia ya kusinzia darasani, wakati
mwalimu anapofundisha na anasinzia ili asiweze kumsikiliza mwalimu na matokeo
yake ni kufeli mitihani, sio kusinzia darasani hata wakati wa kujisomea,
akiingia chumba cha kujisomea usinzia mwanzo hadi mwisho, katika hali hii mtoto
hawezi kufaulu, kafungwa na anahitaji msaada wa maombi ili kubomoa ngome hiyo,
hivyo kama familia inasali vizuri hali hii hutoweka kabisa.
7. Ukiziwi wa kutengeneza.
Watoto wengi waliopata ukiziwi ambao umejitokeza akiwa
shule, anaweza kupona kwa asilimia 100% kwa maombi tu, na watoto hawa
wanafanywa viziwi ili waweze kufeli mitihani yao, wewe mzazi, umezaa watoto
wazima kabisa, ghafla mwanao anakuwa kiziwi wala hushangai, unaridhika tu na
matokeo yake mtoto huyo ufeli kabisa mitihani yake kwa sababu ya kutosikia kile
mwalimu anachofundisha. Watoto wa hivi nimekutana nao katika maombi na wamepona
kabisa.
8. Mwili wa mtoto kukaliwa na nafsi nyingi.
Kuna watoto wengine unafundisha darasani na wewe unaona
unamfundisha mtoto kamili, kumbe sio kweli, unamfundisha Bibi yake au Babu yake
au kitu kingine na mtoto halisi hayupo hapo, yuko kwingine anafundishwa uchawi,
nah ii ni mara chache kugundua ni kwa neema tu. Siku moja nikiwa darasani niliguswa
kuwaambia wanafunzi wapige makofi ya kibunge matatu, walipopiga tu yale makofi
matatu, niliona mtoto mmoja yuko tofauti kama ana nguvu flani na nilichofanya
niliomba darasa zima makofi haya ya kupiga juu ya dawati yaendelee, wakati wakiendelea
yule mtoto aliteseka sana, niliondoka darasani huku nikiwataka wanafunzi
waendelee kupiga makofi, ile napiga hatua chache, yule mwanafunzi darasani
alianza kupiga kelele, nilirudi na kuwaomba wenzake wamtoe nje, nilipomshika
mkono yule Bibi wa kichawi aliyekuwa kavaa mwili wa mtoto, alianza kupiga
kelele na kusema nimekoma, naomba msaada name nilitaka kuvua vema. Binti halisi
yuko wapi, ndipo alisema binti halisi yuko makaburini akifundishwa uchawi, yule
Bibi alieleza binti alipokuwa na kazi aliyokuwa anafanya huko na alieleza wazi
kuwa toka mwezi January au hiyo Mei mtoto halisi hajawai kukanyaga darasani,
ndipo nilipomuita mtoto yule kwa Jina la Yesu kwa nguvu naye alikuja katika
mwili wake na kunieleza kuwa kila alipotoka nyumbani tu Bibi yake alimchukua na
kumpeleka kumfundisha uchawi, na yeye hurudi darasani kukaa nafsi yake, Binti huyo alikombolewa, japo
alipoingia darasa la sita walimtolesha kabisa na wala hakumaliza shule. Hivyo
elimu yake yote iliishia hapo.
9. Kutetemeka wakati wa mitihani, mikono kujaa maji,
kizunguzungu, mkono kuwa mzito.
Hizo zote ni dalili za nguvu za giza na dawa kubwa ni
maombi tu.
10. Ufaulu wa kipepo au nguvu za giza.
Baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakitumia nguvu za giza
katika mitihani yao kwa kuiba akili za watoto wenzao wenye uwezo na kuzitumia
darasani, na maendeleo ya watoto wahusika yanaporomoka kabisa. Na ili mtoto
aliyeibiwa akili aweze kufanya vizuri ni lazimi afunguliwe na akili zake
zikombolewe kwa nguvu ya jina la Yesu.
Basi kwa namna ya pekee niwashukuru wote kwa kusoma
viashiria vya nguvu za giza katika elimu na dawa ya viashiria vyote ni kusali
kwa bidii na mtoto kupata maombi ya kufunguliwa.
Baadhi ya wazazi waliogundua nguvu hii mapema ila njia
wanayotumia sio sahihi ndio maana watoto wao hawajapona mpaka leo, zaidi
niwashauri njooni kwa Yesu na mtaona mambo makubwa bila kutarajia.
Maoni
Chapisha Maoni