Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2023

MADHARA YA VIONGOZI WASHIRIKINA

Picha
  MADHARA YA VIONGOZI WASHIRIKINA Tumsifu Yesu Kristo. Ndugu zangu wote tunajua maana ya madhara, madhara ni uharibifu au athari mbaya tunaweza kuziona baada ya kufanya kitu Fulani na ushirikina ni wazo ambalo halina sababu yenye msingi katika maarifa au mang’amuzi na neno ili hutumiwa kwa kutaja imani ambazo hazina msingi au tunaweza kusema ushirikina ni sayansi iliyotolewa kwa uhusiano kati ya viumbe visivyo hai na wanadamu, uchawi na ushirikina yanaweza kufanana, ushirikina ni kitendo cha kwenda kutafuta msaada wa kiroho au kimwili katika Mamlaka ya giza, namaanisha kwa shetani na mapepo, majini yake yanayofanya kazi kupitia watu wanaoitwa waganga au wachawi. Hivyo leo tuangalie watu hawa ambao ni viongozi wetu na niwashirikina yaani katika utendaji wao wa kazi wanawategemea waganga au wachawi, watu wa namna hii hawawezi kuleta maendeleo katika eneo lao la kazi kwa sababu ya tumia nguvu za giza zaidi wanaweza kusababisha mambo yafuatayo katika maeneo yao ya kazi:- 1.    MIGO

UPAGANI ULIOJIFICHA KATIKA MWAMVULI WA DINI

Picha
  UPAGANI ULIOJIFICHA KATIKA MWAMVULI WA DINI Ndugu zangu wapendwa katika Kristo. Naomba leo kwa pamoja tutafakari huu upagani uliojificha katika mwavuli wa dini. Upagani kwanza ni nini? Mimi naweza kusema upagani ni ile hali ya kuishi bila kujua uwepo wa Mungu, ni hali ya kuishi katika imani isiyofungamana na Mungu mwenyezi, ni hali ya kutegemea miungu wengine, kutomjua Mungu kabisa. Ndugu zangu baada ya kujaribu kuelezea upagani kwa tafsiri yangu, hebu tujiulize tena dini ni nini? Dini ni mkusanyiko wa watu wenye imani moja wanaokusanyika pamoja kwa lengo la kumwabudu Mungu wao, kusali na kuomba pamoja, kuna dini za aina nyingi lakini zote zinakusanyika pamoja kwa imani yao kuongea na Baba yetu aliye mbinguni, na dini uanzia ndani ya familia. Watu wenye dini ujitenga kabisa na mambo ya kipagani utembea na Mungu Muumba nchi na vitu vyote vinavyoonekana na wakiamini Mungu wao anaweza kila kitu, Mungu wao anajitosheleza wala haitaji msaada wowote, hivyo watu wenye dini yaani wen

TUSALI SALA YA ASUBUHI

Picha
  TUSALI SALA YA ASUBUHI   +Kwajina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.   Tuusifu Utatu Mtakatifu wa Mungu mmoja, sasa na siku zote na milele amina. Ee utatu Mtakatifu wa Mwenyezi Mungu; +Baba, +Mwana na +Roho Mtakatifu. Ninasadiki kuwa upo hapa na mahali pote.   Ee Mungu wangu, umeniumba, umenikomboa, umenifanya mkristu, umenizidishia neema zako, umenitayarishia makao yangu mbinguni. Ee Mungu wangu, nakuabudu, nakushukuru, nakuomba toba, nakupenda. Ee Mungu wangu, ninakutolea roho yangu, na mawazo, na maneno, na kazi na furaha, na mateso yangu, uyapokee unipe neema yako nisitende leo dhambi, Amina. ______________________ Ee Baba yetu Mungu mkuu, Umenilinda usiku huu. Nakushukuru kwa moyo, Ee Baba, Mwana na Roho. Nilinde tena siku hii, Niache dhambi, nikutii. Naomba sana Baba wee, Baraka zako nipokee. Bikira safi, Ee Maria Nisipotee nisimamie. Mlinzi mkuu malaika wee, Kwa Mungu wetu niombee Nitake nitende mema tu, Na mwisho nije

ROSARI YA FAMILIA

Picha
  ROSARI YA FAMILIA Tumia Rozari ya kawaida 1.    Anza: K . Ee Mungu unielekezee msaada,          W . Ee Bwana unisaidie hima. Atukuzwe Baba…………………… 2.    Penye Msalaba:   Kanuni ya Imani……………… 3.    Punje kubwa    :   Baba yetu………………… 4.    Punje 3 ndogo :   Salamu Maria……….. x3 5.    Punje kubwa:      Atukuzwe Baba………… 6.   Kwenye Tendo: K . Yesu, Maria na Yosefu ninawapenda; W . Dumisha mapendo na amani katika familia Yangu na familia zote ulimwenguni. 7.    Punje 10 ndogo: K. Yesu, Maria na Yosefu ninawapenda; W . fanya familia yangu iwe takatifu kama familia ya Nazareti   8.    Malizia: Yesu na Maria na Yosefu ninawapenda, ninawaaminisha famila yangu. Ninaomba muwajalie wanafamilia yangu wote katika mwisho wa maisha yao, wajue kuishi pamoja nanyi huko Mbinguni. Amina. PIA UNAWEZA KUTAZAMA VIDEO HIIZI KWA MAFUNDISHO ZAIDI 

MKAKATI WA WACHAWI KUKUZA NA KUENEZA UCHAWI

Picha
  MKAKATI WA WACHAWI KUKUZA NA KUENEZA UCHAWI Tumsifu Yesu Kristo. Ndugu zangu katika Kristu, Katika makala hii napenda kuwashirikisha mkakati wa kukuza na kueneza uchawi. Unaweza usielewe, lakini tunakoelekea tutegemee kuwa na wachawi wengi zaidi, kwa sababu wachawi wamegundua njia bora na nzuri ya kueneza uchawi wao ni kuwafundisha watoto wadogo, na kuwalisha viapo katika Ulimwengu wa giza kiasi kwamba hata mtoto akijitambua anashindwa kujitoa kabisa. Watoto wafuatao wapendwa sana kufundishwa uchawi. 1.     Watoto wa wachawi wenyewe 2.     Watoto Yatima 3.     Watoto ambao wazazi wao wanamafarakano 4.     Watoto ambao ndugu zao ni wachawi 5.     Watoto ambao marafiki na majirani zao ni wachawi na ni rafiki wa familia zao. (kuozeshana watoto wao kwa wao kwa lengo la kukuza uchawi wao.)   ·          Watoto hawa huibiwa nafsi zao, na nafsi zao hizo upelekwa kufundishwa uchawi kwa muda mrefu, na mtoto aliyeibiwa nafsi akilala usiku uota mambo mazito akifanya ikiwa ni