SALA YA KUOMBEA JUMUIYA KWA MAOMBEZI YA MT. PADRI PIO
SALA
YA KUOMBEA JUMUIYA KWA MAOMBEZI YA MT. PADRI PIO
Ee
Mt. Pio leo tunakuja kwako tukijua kwamba kweli wewe ni mtenda miujiza, mmoja
ambaye huko karibu ya Yesu. Tunakuomba utuombee kwa nia zetu mbele ya kiti cha
enzi cha Mwenyezi Mungu kwa maombi yako Jumuiya yetu iwe na mshikamano \ upendo
wa dhati katika kumtumikia Mwenyezi Mungu ndani na nje ya Jumuiya daima
wanajumuiya tutamani kuishi maisha yampendezayo Mwenyezi Mungu katika familia
zetu.
Tunasali
kwa maneno ya Mt. Papa Yohana Paul II, tunakuomba sala zako kwa niaba yetu.
"Adhimu, mnyenyekevu na mpendwa Padri Pio. Tunaomba utufundishe unyenyekevu
wa moyo ili tuweze kuhesabiwa miongoni mwa watoto wadogo wa Injili ambao Baba
aliahidi kuwafundisha siri za ufalme wake. Utusaidie tusali pasipo kukoma, tukiamini
kwamba Mungu anajua tunachohitaji hata kabla ya kumwomba.
Utuombee
tupate macho ya Imani yatakayotusadia kutambua katika maskini na wanaoteseka,
sura halisi ya Yesu. ututunze katika saa ya mahangaiko na majaribu na kama
tukianguka, basi tupate mang`amuzi ya furaha ya sakramenti ya msamaha.
Utuombee
nasi tuwe na moyo kama wako wa upendo kwa Maria, mama wa Yesu na Mama yetu.
Utusindikize katika hija yetu ya hapa duniani kuelekea nchi takatifu ambapo
sisi pia tunamatumaini kufika ili kutafakari milele utukufu wa Baba, Mwana na
roho mtakatifu. Amina".
Mt.
Padri Pio kwa upendo tunasali nawe sala uliyoitunga kwa ajili ya Imani na
matumaini katika huruma ya Mungu. "Ee
Bwana, tunaomba tuwe na matumaini na Imani katika huruma yako ya Kimungu na
ujasiri wa kupokea misalaba na mateso ambayo yanaleta wema tele katika roho
zetu na katika kanisa lako. Utusaidie tukupende wewe kwa Imani na mapendo
makubwa katika Ekaristi Takatifu, na tukuruhusu wewe utende ndani yetu kama
unavyotaka kwa ajili ya utukufu wako mkuu.
Ee
Yesu, moyo unaoabudika sana na chemichemi ya milele ya upendo wa kimungu,
tunakuomba sala yetu ikirimiwe mbele ya ukuu wa kimungu wa Baba yako wa
mbinguni.
Utukufu
wote uwe kwa Baba na kwa Mwana na kwa roho Mtakatifu kama mwanzo na sasa na
siku zote na milele.
Mt.
Padre Pio utuombee. Amina.
Maoni
Chapisha Maoni