SALA KUU YA YESU KRISTO
SALA
KUU YA YESU
Ewe
mkombozi mwenye huruma, uliyekufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, unikinge
na maovu yote yawezayo kunifikia.
Ewe
msulubiwa wa Nazareti, unihurumie leo na kila siku, kwa heshima ya Rabi yetu
Yesu Kristu na kwa heshima ya kufufuka kwake kutakatifu, na kupaa mbinguni kwa
enzi ya Umungu wake na kwa kuwa umeniumba ili nifike mbinguni. Ewe msalaba
mtakatifu wa Kristu unikinge na kifo kibaya cha namna yoyote na unipe uzima
kila siku. Ni hakika kuwa Yesu Kristu alizaliwa katika zizi la ng’ombe siku ya
Noeli, Ewe msalaba mtakatifu wa Yesu Kristu, unikinge na maadui wangu wote. Ni
hakika kuwa wafalme watatu wenye busara walileta zawadi zao kwa siku ya kumi na
tatu tangu kuzaliwa kwake Kristu. Ni hakika kuwa Yesu Kristu alisulubiwa
msalabani kwenye kilima cha Kalvaroo siku ya Ijumaa. Ni hakika kuwa alipaa
mbinguni. Heshima ya yesu itaniondolea maadui wangu niwaonao na nisiowaona leo
na siku zote.
Ewe
Yesu mwema unihurumie. Mama na Yosefu mlliyemwondoa Yesu msalabani na kumzika
mniombee, Ewe Yesu mwema unipe neema niubebe msalaba wangu kwa uvumilivu hasa
ninapokuwa na mateso ndipo niepukane na kila aina ya dhambi leo na siku zote.
Heshima
ya Rabi wetu Yesu Kristu na mateso yake matakatifu. Ishara ya msalaba wake
mtakatifu na unyenyekevu wake.
Bikira
Maria, Mama Mlezi na mwombezi wa watakatifu wote unisaidie. AMINA.
MAELEZO YA SALA KUU YA YESU
Salah
ii ilikutwa ndani ya kaburi la Rabi wetu Yesu Kristu, katika mwaka 8035, Sala
hii alipewa mfalme Charles na Baba Mtakatifu alipokuwa anakwenda vitani ili
imsaidie mfalme huyo. Wale wanaokaa nayo na kuisoma na kuitunza kila siku
hawawezi kufa kifo cha ghafla, au kufa kwenye maji, hata kupewa uchawi. Yeyote
yule anayetembea na Salah ii asiopoge umeme au mvua, radi, kufa ghafla. Iwapo
itasomwa alipo mwanamke mwenye mimba atazaa salama na kuwa mzuri na mchangamfu
na sala hii iwekwe mkono wa kulia wa mtoto aliyezaliwa. Mtoto huyo hatapata
taabu maisha yake yote, Ikiwa kuna mtu anayeanguka kifafa, ukimsomea kwa makini
na utulivu sala hii, ataamka na kumshukuru muumba. Nyumba yoyote yenye sala hii
itakuwa nyumba yenye Baraka.
Ukubali
hayo yote kama unavyokubali maandiko matakatifu ya waandishi wa Injili mtu
yeyote anayedharau sala hii atapatilizwa wale wanaotembea nayo sala hii na
kuisoma kila siku watajulishwa siku tatu zinazotangulia kufa kwao.
Naamini
maelezo ya sala hii, aisali nawe utaona makuu kadri ya mapenzi ya Mungu na
ushuhuda wake mimi ninao.
Namshukuru Mungu kwa nguvu zake ndani
ya sala hii.
Mt.
Yuda Tadeo, Mtume mtukufu, Mtumishi mwaminifu na rafiki wa Yesu. Jina la yule
msaliti aliyemwuza Yesu limewafanya wengi wakusahau, walakini kanisa zima
linakuheshimu na kukuomba kama msaidizi katika mashaka makubwa na katika mambo
yasiyo na matumaini tena.
Uniombee
mimi mnyonge – ninakuomba utumie uwezo ule uliojaliwa wa kuleta upesi msaada
kwa watu walioukosa unisaidie sasa katika mahitaji yangu, nipate kitulizo na
msaada wa mbinguni katika hazina zangu, masumbuko na mateso hasa (Taja shida
zako) pia ili niweze kumsifu Mungu nawe na wateule wote milele.
Mtakatifu
Yuda Tadei, uwaombe watu wote wanaokuheshimu na kukuomba msaada.
Moyo
mtakatifu wa Yesu, rafiki mpenzi wa Yuda Tadei nakutumainia.
(Mwisho
Sali Baba yetu, Salamu Maria na atukuzwe.) Amina.
WARIDI SALA YA NOVENA.
Ee
Mtakatifu Terezia mdogo wa mtoto Yesu nakuomba unichumie waridi kutoka kwenye
bustani ya mbinguni na unitumie kama ujumbe wa upendo. Ewe waridi dogo la yesu,
umwombe Mungu anijalie neema hii ninayoiweka mikononi mwako.
…………………….
Mtakatifu Terezia, kama wewe unisaidie mimi pia niwamini upendo wa Mungu kwangu
ili kila siku niige njia yako ndogo. AMINA
SALA YA PEKEE KWA MTAKATIFU YOSEFU
Ee
Mt. Yosefu, uliye na ulinzi mkubwa imara na haraka sana mbele ya kiti cha
Mungu. Ninakuwekea nia zangu zote na mambo yangu yote, unishughulikie Ee Mt.
Yosefu, nakusihi, unisaidie kwa maombezi yako yenye nguvu na unipatie kutoka
kwa mwanao Mungu, Baraka zote za roho na mwili, kwa njia ya Kristu mwana wetu,
hivi kwamba nikiisha kuupata msaada wako wa mbinguni ningali hapa duniani,
niweze kutoa sifa na shukrani zangu.
AMINA.
SALA YA KULIPIA MAKOSA YA KILA SIKU
Ee
Mungu Baba wa milele, ninakutolea moyo mtakatifu wa Yesu kristu, mwanao mpenzi,
pamoja na upendo wake, mateso yake na stahili zake zote.
Kwanza
– Kwa kulipia dhambi zangu zote nilizotenda siku ya leo na katika maisha yangu
yote. Atukuzwe Baba.
Pili
– Kwa kuyatakasa matendo mema, niliyopaswa kuyafanya, name nikakosa kuyatimiza
siku ya leo na katika maisha yangu yote. Atukuzwe Baba
Tatu
– Kwa kufidia matendo yote mema, niliyopaswa kuyafanya, nami nikakosa
kuyatimiza siku ya leo na katika maisha yangu yote. Atukuzwe Baba
Baba
wa milele, kwa njia ya moyo safi wa Maria, Binti wako mteule milele,
ninakushukuru kwa neema zote ulizonijalia siku ya leo na katika maisha yangu
yote.
Atukuzwe
Baba……………
Salamu
Maria ……………...
13.09.1935
Tumia
Rosari ya kawaida.
(a) Anza hivi.
Baba yetu …………………
Salamu Maria …………….
Nasadiki ……………………
(b) Kwenye vyemba vya
"Baba kyetu Sali hivi"
(Baba wa Milele, ninakutolea mwili na damu, Roho na
umungu vya Mwanao mpenzi, Bwana wetu Yesu Kristu, kwa kulipia dhambi zetu na
dhambi za dunia nzima.
(c) Kwenye vyemba vya "Salamu Maria" sema
"kwa ajili ya mateso makali ya Yesu utuhurumie sisi na dunia nzima."
x 10
(d) Mwisho, sema maneno haya yafuatayo mara tatu "Mungu
Mtakatifu, Mtakatifu mwenye nguvu, Mtakatifu asiyeweza kufa utuhurumie sisi na
dunia nzima. x 3 AMINA
(e) KUMBUKUMBU MAALUMU – Bwana wetu Yesu Kristu anataka tufanye mara nyingi,
Novena ya Rosari ya Huruma ya Mungu,
Novena ya siku (9) tisa, tisa. Kwa Novena ya Rosari hii, tutapata kila neema
tuombayo, bora tu ipatane na mapenzi ya Mungu.
TENA> Yeyote afanyaye Novena ya huruma ya Mungu hana budi
kusali pia Rosari ya huruma ya Mungu, kwa matayarisho ya sikukuu ya huruma ya
Mungu au wakati mwingine wowote maishani ahadi za rosary hii ni kubwa na za
pekee.
Bwana
wetu alimwambia Sir. Faustina (Baada ya 13.09.1935) heri yake mtu yule ambaye
katika maisha yake anajizoeza kuikimbilia Huruma ya Mungu, kwa maana siku ya
hukumu ya mwisho. Hatahukumiwa. Huruma ya Mungu itamkinga.
Mwanangu,
wahimize watu waisali hii Rosari ya Huruma niliyokufundisha. Kwa kuisali Rosali
hii nitawapa kila neema watakayo iomba. Hata wakosefu wagumu, wakuisali mtajaza
roho zao kwa Amani na nitawajalia kifo chema wanaposali Rosali hii karibu na
mtu anayekufa, mimi nitasimama kati ya roho hiyo na Baba yangu, si kama Hakimu
mwenye haki, bali kama mwokozi wa wenye huruma.
SIKUKUU YA HURUMA YA MUNGU
Bwana
Yesu alimwambia Sir. Faustina nataka Jumapili ya kwanza baada ya pasaka iwe
sikukuu ya Huruma yangu. Siku hiyo
kilindi cha huruma yangu kutakuwa wazi kwa wote.
SAA YA HURUMA KUU YA MUNGU (Saa tisa
Alasiri)
Bwana
alimwambia Sir. Faustina.
Itiwapo
saa tisa, omba huruma ya Mungu (Huruma yangu) hasa kwa ajili ya wakosefu. Nawe
haidhulu hata kwa dakika chache tu.
HABARI YA SALA HIZI
Sala
hizi zote nilizitoa katika kitabu cha Sala cha Mawaridi na kukopi baadhi ya
sala ambazo niliona zinanifaa yapata miaka Ishirini na mbili sasa iliyopita,
nilizikopi toka tarehe 03.10.1993, na daftari la awali la Sala hizi limezeeka
na leo tarehe 26 Jumatatu Desemba 2022 nimezihamisha tena katika blog hii.
FAIDA YA SALA HIZI
Katika
kipindi chote cha miaka ishirini na mbili hadi sasa, nimeona ukweli ulio katika
sala kuu ya Yesu. na Rosari kuu ya huruma ya Mungu. Hivyo Sali sala zote kadri
ya Imani yako na Mungu atakusaidia. AMINA
Maoni
Chapisha Maoni