SALA NA FAMILIA
Tumsifu Yesu Kristo!
Ndugu
zangu wapendwa ni wazi kila mtu ametoka katika familia na kila mtu anayo
familia.
Tunajua
wazi tunfamilia za aina mbalimbali yaani iwe ni familia ya Baba, Mama na watoto
au familia ya Mama na watoto au familia ya Baba na watoto au familia ya watoto
tu wanaojilea wenyewe, zote hizo ni familia.
Mzazi
Baba au Mama ni kiongozi katika familia yako, yawezekana unatimiza majukumu
yote muhimu ya familia yako kwa kuhakikisha watoto wako wanapata Chakula bora,
Elimu bora na Maradhi bora kabisa, yote haya ni jambo jema kabisa. Lakini
katika swala la Imani au kuwasisitiza watoto kusali ukajisahau kidogo, kwa
misingi hiyo, Leo nakuja kukukumbusha umuhimu wa kumjengea mtoto wako Hofu ya
Mungu, Utii kwa Mungu, mahusiano mema na Mungu wake, kwa kufanya hivyo utakuwa
umetimiza wajibu vema ndani ya familia yako.
Lazima
ukumbuke mambo yafuatayo:-
1. MALEZI YA MITANDAONI
Kumbuka hivi sasa kuna malezi mazuri na malezi mabaya
yanayotolewa katika mtandao, ambayo yanaweza kukuharibia mtoto kabisa au
kumjenga mtoto, na ili kushinda vita hivi vya malezi ya mtandaoni lazima mtoto
wako hampende Mungu wake, awe na hofu ya Mungu.
2. TABIA CHAFU KATIKA
JAMII INAYOMZUNGUKA
Ila mtoto wako aweze kushinda tabia chafu inayomzunguka
lazima awe na nguvu ya Mungu na nguvu ya Mungu anaipata katika sala. Hivyo kama
familia lazima kusali.
3. ULINZI WA FAMILIA
Kuna baadhi ya familia zinapata mashambulizi ya kiroho
kwa sababu hazisali tu, na mashambulizi haya ni pamoja na Magonjwa yenye
kulenga kudhoofisha Uchumi wa familia, watoto kukataa shule bila sababu ya
msingi. Ndoa kuvunjika, watoto kuzaliwa na kupoteza maisha katika hali isiyo ya
kawaida yote hayo ni kwasababu ya familia kukosa ulinzi, ni familia kumuweka
Mungu mbali, ni familia kutokusali.
4. KUWALINDA WATOTO WAKO
NA NGUVU ZA GIZA
Kumbuka wazi Mungu wetu adanganyi wala adanganyiki, na
wala haitaji msaada wowote toka kwa miungu unayoijua wewe, hivyo ili uweze
kuilinda familia yako vyema unatakiwa kuwahimiza watoto wako kusali kwa bidii
na kusoma kwa bidii, na endapo watoto wako wanaumwa wapeleke hospitali kwa
matibabu na waombee au wapeleke pia kwa Yesu wa Ekaristu, tumia matibabu ya aina mbili ya hospitali na maombi ili
dawa anazotumia kwa Baraka za Mungu zikatende kazi njema.
Kuna magonjwa mengi siku hizi ya nguvu za giza na
yanafanana kabisa na magonjwa yasiyo ya nguvu za giza na bila kusali hauwezi
kamwe kuyatofautisha. Na magonjwa haya yamekuwa yakiporomosha Uchumi wa familia
na kufanya familia kuwa maskini kabisa, mfano wa Magonjwa hayo ni kama vile
Ø Mtoto kuugua au kupata tatizo la upungufu wa damu.
Ø Kuugua kisukari
Ø Kuugua macho
Ø Maumivu ya kichwa n.k
Magonjwa
haya yapo kweli lakini mengine niyakutengenezwa katika Ulimwengu wa giza, hivyo
kama familia haisali na Adui anaiwinda familia hiyo ataweza kuisambaratisha
kabisa kwa urahisi kwa maana iko mbali na Mungu.
Hivyo
kama wazazi lazima kuweka utaratibu wa sala ndani ya familia zetu, kukaa mbali
na Mungu ni kujidanganya. Familia iliyo salama lazima itembee na Mungu sio
pesa.
Familia
na sala ni nguvu ya ushindi katika malezi, katika safari yetu ya hapa duniani,
kwa neema ya Mungu niwatakiye wanafamilia wote kutembea na nguvu ya Mungu ndani
ya familia zetu.
Mungu
awabariki sana.
Mwl.
Julius Theophil Mmbaga
Mtumishi
ndani ya Familia
0766500747
TAZAMA VIDEO HII UPATE KUJIFUNZA ZAIDI
Maoni
Chapisha Maoni