SALA KUU YA YESU KRISTO
SALA KUU YA YESU Ewe mkombozi mwenye huruma, uliyekufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, unikinge na maovu yote yawezayo kunifikia. Ewe msulubiwa wa Nazareti, unihurumie leo na kila siku, kwa heshima ya Rabi yetu Yesu Kristu na kwa heshima ya kufufuka kwake kutakatifu, na kupaa mbinguni kwa enzi ya Umungu wake na kwa kuwa umeniumba ili nifike mbinguni. Ewe msalaba mtakatifu wa Kristu unikinge na kifo kibaya cha namna yoyote na unipe uzima kila siku. Ni hakika kuwa Yesu Kristu alizaliwa katika zizi la ng’ombe siku ya Noeli, Ewe msalaba mtakatifu wa Yesu Kristu, unikinge na maadui wangu wote. Ni hakika kuwa wafalme watatu wenye busara walileta zawadi zao kwa siku ya kumi na tatu tangu kuzaliwa kwake Kristu. Ni hakika kuwa Yesu Kristu alisulubiwa msalabani kwenye kilima cha Kalvaroo siku ya Ijumaa. Ni hakika kuwa alipaa mbinguni. Heshima ya yesu itaniondolea maadui wangu niwaonao na nisiowaona leo na siku zote. Ewe Yesu mwema unihurumie. Mama na Yosefu mlliyemwondoa Yesu msa...