HISTORIA YA MAISHA YA BIKIRA MARIA
HISTORIA YA MAISHA YA BIKIRA MARIA MAISHA YA WAZAZI WA BIKIRA MARIA Mnamo karne ya pili kabla ya kuzaliwa kwake Bwana wetu Yesu kristo. Wazazi wa Bikira Maria walijulikana katika Kanisa kwa majina ya JOAKIMU na ANNA. Hata ilipofika karne ya nne, Wakristu wa kanisa la Mashariki walikuwa tayari wameshazoea kuwaheshimu wazazi hawa. Mwaka 1548 Kanisa Katoliki lilianza rasmi kusherekea sikukuu ya wazazi wa Mungu, Katika kalenda ya Kanisa sikukuu ya Watakatifu hawa huadhimishwa tarehe 26 Julai kila mwaka. BABA MZAZI WA BIKIRA MARIA Joakimu ndiye Baba mzazi wa Bikira Maria, Baba huyu alikuwa wa kabila la Yuda na Ukoo wa Mfalme Daudi. Jina Joakimu lina maana ya Matayarisho kwa ajili ya Bwana ; au Bwana anatayarisha. Mtakatifu huyu aliishi Nazareti iliyoko Galilaya. MAMA MZAZI WA BIKIRA MARIA Anna ndiye mzazi wa Bikira Maria, Mama huyu alizaliwa katika ukoo wa Haruni Kuhani Mkuu wa kabila la Yuda. Jina la Anna lina maana ya Neema au Enye Neema. Mama huyu nyumbani kwao kulikuw...