Machapisho

Mwl.JULIUS THEOPHIL MMBAGA

Picha
  Mimi ni Mkatoliki:Namshukuru Mungu Muumba Mbingu na nchi na vitu vyote vinavyoonekana kwa namna alivyoweza kubadilisha maisha yangu na familia yangu na kunifanya nimtumikiye kama chombo chake kwa ajili ya watu wenye shida mbalimbali. Nashuhudia huruma ya Mungu kwa watu wenye shida mbalimbali na wanaomtumaini Mungu jinsi wanavyopona na kumrudisha Mungu sifa na utukufu. Ni mwaka wa tano sasa nafanya huduma za uponyaji na ufunguliwaji.Asante Yesu kwa Uwepo wako ndani fumbo takatifu la Mkate na divai(EKARISTI TAKATIFU). Asante Yesu kwa kunitumia tu kama chombo chako,ukiwa na imani kwa Mungu hakuna kinachoshindika, nafanya maombia pia kwa njia ya simu [0766500747] na Mungu hutenda, Mungu akubariki sana.

HISTORIA YA MAISHA YA BIKIRA MARIA

Picha
  HISTORIA YA MAISHA YA BIKIRA MARIA MAISHA YA WAZAZI WA BIKIRA MARIA Mnamo karne ya pili kabla ya kuzaliwa kwake Bwana wetu Yesu kristo. Wazazi wa Bikira Maria walijulikana katika Kanisa kwa majina ya JOAKIMU na ANNA. Hata ilipofika karne ya nne, Wakristu wa kanisa la Mashariki walikuwa tayari wameshazoea kuwaheshimu wazazi hawa. Mwaka 1548 Kanisa Katoliki lilianza rasmi kusherekea sikukuu ya wazazi wa Mungu, Katika kalenda ya Kanisa sikukuu ya Watakatifu hawa huadhimishwa tarehe 26 Julai kila mwaka. BABA MZAZI WA BIKIRA MARIA Joakimu ndiye Baba mzazi wa Bikira Maria, Baba huyu alikuwa wa kabila la Yuda na Ukoo wa Mfalme Daudi. Jina Joakimu lina maana ya Matayarisho kwa ajili ya Bwana ; au Bwana anatayarisha. Mtakatifu huyu aliishi Nazareti iliyoko Galilaya. MAMA MZAZI WA BIKIRA MARIA Anna ndiye mzazi wa Bikira Maria, Mama huyu alizaliwa katika ukoo wa Haruni Kuhani Mkuu wa kabila la Yuda. Jina la Anna lina maana ya Neema au Enye Neema. Mama huyu nyumbani kwao kulikuw...

CHANGAMOTO YA NDOTO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO

Picha
  CHANGAMOTO YA NDOTO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO Tumsifu Yesu Kristu, Ndugu yangu katika Makala hii napenda leo kujadili juu ya changamoto ya ndoto katika ulimwengu wa roho. Ninaposema changamoto ya ndoto katika Ulimwengu wa roho namaanisha ni hali ya mtu kuota ndoto ambazo zinafanana sana na uhalisi wake katika hali ya kawaida, yani unaota ndoto ambayo wewe mwenyewe unaona au unahisi kabisa kitu hichi ni kweli kimefanyika, mfano wa ndoto hizi ni 1)     Unaota unakula nyama mbichi na unapohamka ukitafakari hiyo ndoto na ukigusa meno yako unawez kukuta mabaki halisi ya nyama katika kinywa chako.   2)     Unaota unakula kweli na ukiamka asubuhi umeshiba kabisa wala huitaji chakula chochote.   3)     Unaota unakimbizwa, na unakimbia kweli, ukizinduka katika ndoto unajikuta ni mtu mwenye hofu na unahema kweli na kila tukio unalikumbuka vema.   4)       Unaota huko katikati ya watu waliovaa...